Usiku wa April 8, 2016 Star Times iliwakutanisha wadau wa soka Tanzania na Nwankwo Kanu mkali wa zamani wa Arsenal, Inter Milan, Ajax na timu ya taifa ya Nigeria The Super Eagles kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya soka la Tanzania pamoja na Afrika kwa ujumla.
Katika hotuba yake fupi aliyoitoa kwenye ukumbi wa Serena Hotel, Kanu amesema mafanikio yoyote ya soka yanaletwa na vijana.
“Watoto wadogo wakiandaliwa katika misingi bora, watakuwa wachezaji bora wa baadaye na kusaidia mataifa yao. Ni vyema kujenga vituo vingi vya kulelea vijana wenye vipaji na kuwatunza ili kuwafanya wawe baora baadaye”.
Lakini akasisitiza kwamba, suala la afya ni muhimu katika soka hususan kwa vijana ambao wanatakiwa kulelewa na kutuzwa kimichezo pamoja na kujali afya zao.