Kocha Mkuu wa Al Ahly ya Misri ambayo kesho itashuka kwenye uwanjani kuumana na wenyeji wao Yanga Martin Jol ametoa kali akisema kila anapopita wanaonyeshwa wanapigwa tatu ishara ambayo itabidi wajiandae.
Jol amesema hilo jioni hii wakati Al Ahly ikifanya mazoezi yake ya mwisho katikia uwanja wa Taifa ambapo amesema kila kitu kipo sawa kwao tayari kwa kukabiliana na Yanga.
Amesema amefurahia kukuta Uwanja mzuri wa kisasa ambaop ndiyo utatumika kwa mchezo jambo ambalo hakulitegemea kabloa ya kuuona.
“Watu wanatuonyesha tatu kila tunapopita ukiona hilo lazima uwe tayari na sisi tumejiandaa katika hilo changamoto niliyonayo ni kuchagua wachezaji watakaoanza,” amesema Jol.
“Jmabo zuri nililolifurahia Tanzania watu ni wakarimu sana ni nchi nzuri nafikiria kuja tena hata huu uwanja ni mzuri nimeupenda nyasi zake zipo sawa sikutegemea hili.”