Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

WAKATI, THOMAS ULIMWENGU AKIWA NJIA PANDA, JUMA LIUZIO KUCHEZA 8 BORA MABINGWA AFRIKA

$
0
0
Juma  Liuzio-Mshambuliaji wa ZESCO United ya Zambia
Juma Liuzio-Mshambuliaji wa Zesco United ya Zambia

Na Baraka Mbolembole

Mshambulizi wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Juma Ndanda Liuzio anaamini kwamba ushindi wa 3-1 ugenini dhidi ya Stade Malien utaipeleka timu yake ya Zesco United katika hatua ya makundi ya ‘Ligi ya mabingwa’ Afrika msimu huu.

Mabingwa hao wa Zambia wanahitaji sare au ushindi wa aina yoyote kufuzu kwa nane bora msimu huu. Liuzio ambaye ataorodheshwa katika timu yake kama itafuzu kwa hatua inayofuata alikuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi minne lakini sasa yuko fiti na tayari amecheza mchezo mmoja wa timu yake katika ligi kuu Zambia ambayo ipo katika mzunguko wake wa kwanza.

“Tuna uhakika wa kufuzu kwa hatua inayofuata baada ya kupata matokeo mazuri katika mchezo wa kwanza nchini Mali”, anasema straika huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar wakati nilipofanya naye mahojiano mafupi akiwa nchini Zambia.

“Sijafanikiwa kucheza mchezo wowote katika ligi ya mabingwa kwani sikuorodheshwa katika kikosi kutokana na majeraha ya nyama za paja ambayo niliyapata mwezi Novemba (2015.) Nitacheza hatua inayofuata kwani kwa sasa naendelea vizuri na tayari nipo kikosini”, anasema Luizio ambaye yuko nje ya timu ya Taifa tangu katikati ya mwaka uliopita.

Baada ya TP Mazembe kufungwa 2-0 na Wydad Casablanca ya Morocco ni wazi mabingwa hao watetezi wana kazi kubwa kuhakikisha wanafuzu kwa hatua ya makundi.

Kama watashindwa kufuzu inamaanisha kwamba mshambulizi mwingine wa Taifa Stars, Thomas Ulimwengu atakwama kucheza robo fainali ya mabingwa Afrika lakini kuna uwezekano mkubwa kwa Watanzania kumuona kijana wao mwingine (Liuzio) akifanya mambo katika michuano hiyo mikubwa zaidi ngazi ya vilabu barani Afrika.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>