Real Madrid bado wanaamini wanaweza kubadili matokeo ya 2-0 dhidi ya Wolfsburg na kufanikiwa kuendelea mbele katika michuano ya klabu bingwa ya ulaya.
Ukiachana na mzimu wa historia ya miaka 29 ya kushindwa kubadili matokeo, takwimu za timu chini ya usimamizi wa Zidane katika uwanja wa Santiago Bernabeu msimu huu zinaongeza uzito wa hoja ya Madrid kuweza kubadili matokeo na kufuzu.
Tangu Zidane alipowasili Bernabeu, Real Madrid wamekuwa na wastani wa kufunga angalau magoli manne 4.1 katika dimba lao la nyumbani.
Endapo watafanikiwa kuendelea na rekodi yao hiyo leo usiku basi tutegemee kuona Los Blancos wakifuzu na akuwemo miongoni mwa timu nne katika droo ya nusu fainali Ijumaa hii.
Zidane ameiongoza Madrid katika mechi 9 katika uwanja wa Santiago Bernabeu na matokeo katika mechi 7 kati ya 9 zilikuwa za ushindi. Matokeo ambayo kwa upekee yalikuwa tofauti na ushindi na kipigo cha 0-1 vs Atletico na wakati ushindi wa 4-2 VS Wolfsburg leo ushindi kama ilivyokuwa ushindi wao wa 4-2 vs Athletic, utasawasaidia Wajerumani kufuzu. Ushindi wa 2-0 kwa Madrid utamaanisha mchezo utaenda extra time.
Kwa upande mwingine wa shilingi hivi karibuni Madrid wamekuwa wakishindwa kubadili matokeo katika mechi za ulaya. Mara ya mwisho wa Madrid kufuzu baada ya kufungwa kwa tofauti ya magoli katika mchezo wa kwanza ilikuwa mwaka 1987, vs Red Belgrade ya Yugoslavia. katika miaka ya hivi karibuni inabidi urudi nyuma mpaka 2002 ili kuweza kuona Madrid wakibadili matokeo katika UCL baada ya kupata hasi katika mchezo wa kwanza, walifanikiwa kuifunga 2-0 Bayern Munich @Santiago Bernabeu baada ya kukubali kipigo cha 2-1 nyumbani kwa Bayern.