
Ukiachana na matokeo ya Yanga kuifunga Mwadui FC kwa magoli 2-1 kwenye mchezo uliochezwa April 13, 2016 kwenye uwanja wa taifa, kitu kingine kilichokuwa gumzo uwanjani walikuwa ni warembo kadhaa ambao waliteka ‘attention’ ya baadhi ya mashabiki waliokuwepo uwanjani kushuhudia pambano hilo.
Star wa Bongo Movies maarufu kwa jina la Kabula alikuwepo uwanjani akiwa ameambatana na mrembo mwingine ambaye hakufahamika jina lake mara moja.

Mashabiki wengi walionekana kuwashangaa warembo hao inawezekana kutokana na style walizokuwa wamenyuka walipokwenda uwanja wa taifa kushuhudia pambano la VPL.

Jicho la mtandao huu lililokuwepo uwanja wa taifa liliwanasa warembo wengine wawili ambao pia walikuwa kivutio uwanjani hasa pale walipoamua ku-kanga photo ‘selfie’ wakati wapo jukwaani wakifurahia burudani kutoka kwa Yanga na Mwadui.
Mara kadhaa Kabula amekuwa akihudhuria uwanjani kushuhudia michezo mbalimbali inayopigwa kwenye uwanja wa taifa lakini mara nyingi huonekana kwenye mechi zinazoihusu klabu ya Yanga.