“Ngassa alitupongeza kwa namna tulivyocheza kipindi cha kwanza lakini akasema ni lazima tujitahidi kupata goli mapema tukirudi kipindi cha pili kwasababu Mtibwa wanacheza vizuri na endapo hatutawafunga mapema hawataruhu goli dakika za majeruhi kwasababu watajilinda wasipoteze mchezo bali watataka kuondoka na pointi moja”, amesema mmchezaji mmoja wa Yanga ambaye hakupenda kutajwa jina lake.
Kitu kilichowavutia wachezaji wa Yanga ni pale nyota huyo anayekipiga Free State Stars ya Afrika Kusini alimkabidhi Haruna Niyonzima pair moja ya viatu vya mpira kama zawadi, Ngassa na Niyonzima ni washkaji wa muda mrefu na inasemekana sababu nyingine kubwa ya Niyonzima kukubali kusajiliwa Yanga ilikuwa ni kucheza pamoja na Ngassa.
www.shaffihdauda.co.tz ilifanya jitihada za kuzungumza na nyota huyo lakini mazingira hayakuwa rafiki kuweza kufanyanae mahojiano.
Ngassa ambaye aliwahi kuvitumikia pia vilabu vya Kagera Sugar, Azam FC na Simba SC kwa nyakati tofauti amerejea nchini kutokana na kufiwa na mdogoake na leo (Jumapili Aril 17) amesafiri kuelekea nyumbani kwao Mwanza kwa ajili ya kuhudhuria msiba huo.