Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

MESSI AINGIA TENA KWENYE VITABU VYA REKODI

$
0
0

Messi 500

Superstar wa Argentina Lionel Messi usiku wa jana amefikisha magoli 500 katika maisha yake ya soka aliyoifungia klabu yake na timu yake ya taifa baada ya kufunga bao moja wakati Barca ikilala 2-1 nyumbani mbele ya Valencia.

Nyota huyo mwenye miaka 28 alimaliza ukame wa kucheza dakika 515 bila ya kufunga bao kufuatia kufunga goli hilo akiwa umbali wa mita 10 toka alipo golikipa wa Diego Alves wa Valencia.

Hata hivyo haukuwa usiku wa sherehe kwa Barcelona ambao walijikuta wakidondosha tena pointi kwenye La Liga na kufanya mbo za ubingwa wa ligi hiyo kuwa wazi kwa timu zote tatu (Barcelona, Atletico Madrid na Real Madrid).

Leo Messi hata hakushangilia bao hilo ambalo limemuweka kwenye vitabu vya rekodi kutokana na kikosi Luis Enrique kupoteza mchezo huo wakati kilikuwa kikihitaji pointi tatu zilizokuwa muhimu kwao.

Messi 500 a

Kipigo cha bao 2-1 kwenye uwanja wao wa nyumbani dhidi ya Valencia kinafanya Real Madrid kuwa nyuma ya Atletico Madrid na Barcelona kwa pointi moja (Barcelona na Atletico Madrid zinalingana pointi) huku zikiwa zimesalia mechi tano ili kumalizika.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>