Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

SAMATTA AISHUHUDIA GENK IKICHAPWA NYUMBANI

$
0
0

IMG_0989

Nyota wa Tanzania Mwana Samatta usiku ya Jumapili April 24 alikuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha Genk kilichocheza shuks uwanjani kuikabili klabu ya Gent mchezo uliomalizika kwa Genk kunyukwa bao 2-1.

Mbwana Samatta amepata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Peter Maes kilichokuwa kwenye uwanja wa nyumbani Cristal Arena kucheza mchezo wa Belgian Pro League Group stage.

Genk walianza kupata bao lao kupitia kwa Leon Bailey dakika ya 16 kipindi cha kwanza lakini lilidumu kwa dakika saba kwani dakika ya 23 Thomas Matton akaisawazishia Gent.

Katika mchezo huo, Samatta alishindwa kurejea uwanjani kipindi cha pili baada ya kuumia pua na nafasi yake kuchukuliwa Nikolaos Karelis aliyeanzia kwenye benchi.

Wakati kila mtu akiamini mchezo huo utamalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1, Gent walipata mkwaju wa penati dakika ya 90 baada ya golikipa wa Genk kumchezea madhambi mshambuliaji wa Gent na penati hiyo kuwekwa kambani na Renato Neto na kuipa ushindi Gent.

Samatta ameendelea kuaminiwa na kocha wake Peter Maes na ameanza kupewa nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza. Samatta alifunga goli kwenye mchezo uliopita wakati timu yake ikiibuka na ushindi wa magoli 4-2 dhidi ya Club Brugge.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>