Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

SPURS YAIWASHIA LEICESTER TAA YA KIJANI UBINGWA WA EPL

$
0
0

Spurs-ubingwa

Mashabiki wa Leicester City watakuwa wakiimba  na kulishangilia jina la Tony Pulis kwa muda wote baada ya kukiongoza kikosi chake cha West Brom kuwang’ang’ania Spurs na kuwalazimisha sare ya kufungana goli 1-1 kwenye uwanja wa White Hart Lane.

Kikosi chake kilielemewa kipindi cha kwanza lakini baada ya mapumziko kilirejea uwanjani kwa kasi licha ya kuwa nyuma kwa goli 1-0. Wakati huo Spurs walikuwa na matumaini kwamba ushindi kwenye mchezo huo ungepunguza gap la pointi kati yao na Leicester katika kuwania mbio za ubingwa wa EPL.

Lakini kipindi cha pili mambo yalikuwa magumu kwa Spurs baada ya West Brom kusawazisha bao hilo. Sare hiyo inatoa mwanya kwa Leicester kutangaza ubingwa endapo itashinda mchezo wake dhidi ya Manchester United weekend hii.

The Foxes wananafasi kubwa ya kushinda taji la Premier League wakihitaji ushindi kwenye mchezo mmoja kati ya mechi tatu zilizosalia.

Leicester City wanapointi 76 wakati wapinzani wao wa karibu Spurs wakiwa na pointi 69 huku timu zote zikiwa simesaliwa na mechi tatu. Endapo Leicester wakishinda mchezo mmoja kati ya hiyo, watafikisha pointi 79 ambazo haziwezi kufikiwa na Spurs hata kama itashinda mechi zote. Kama Tottenham itashinda mechi zote zilizosalia itafikisha pointi 78.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles