Namshkuru mungu nimefika salama hapa Ujerumani Frankfurt kwa ajili ya ziara yangu kwenye ligi ya Bundesliga. Baada ya kufika tu ratiba yangu ikanipeleka kwenye workshop ambayo imeandaliwa na chama cha soka cha ujerumani. Hapa nimekutana na waandishi nguli wa michezo kutoka barani Africa.
Safari yangu hii ambayo ipo chini ya StarTimes ambacho ndicho king’amuzi kinachokuwezesha kuangalia ligi hii yenye kasi na mashabiki wanaojaza viwanja kwenye kila mechi. Endelea kuwa na mimi nitakujulisha kila kinachotokea huku.