Katika kile kinachoonyesha ni kujipanga vyema, kampuni nguli za mawasiliano nchini Huawei na Tigo wameungana kukukufikishia huduma kwa gharama nafuu na haraka zaidi.
Tigo na Huawei wameungana kukuletea simu za mkononi aina ya Huawei Y360 ambazo zitakua zikiuzwa katika maduka ya Tigo nchi nzima.
Katika kujua watanzania wamelipokeaje hili, nilitembelea maduka kadhaa ya Tigo jijini Dar es Salaam kuzungmza na wateja wao.
Aboubakar Msami mkazi wa Temeke anasema
‘Ni simu nzuri ya kipekee, bei yake ni nafuu na zaidi unarudishiwa pesa hiyo kama vifurushi kwa miezi sita. Nadhani ushirikiano huu wa makampuni uwepo mara kwa mara ili kutunufaisha zaidi’
Nae Antony Shirima anayejishughulisha na uuzaji na utangenezaji wa simu Kariakoo jijini Dar es Salaam alikua na haya ya kusema.
‘Niliposikia wanauza hii simu 160,000 nilihisi ni kama utani fulani, huwezi kupata smartphone yenye Android 4.4.2, kamera megapixel 5, ya mbele 2 na kioo cha inchi nne kwa bei hiyo labda ziwe zile za watu wenye macho madogo’