Swansea City imeitoa nishai Liverpool na kujihakikishia maisha kwenye Premier League ndani ya msimu ujao.
Andre Ayew alianza kutupia bao la kwanza kwa kichwa kabla ya goli linguine kutoka kwa Jack Cork na kuiweka Swansea mbele kipindi cha kwanza kwa magoli 2-0.
Goli la Christian Benteke ililifufua matumani kwa Liverpool kipindi cha pili lakini la pili la Andre Ayew ambalo lilikuwa ni la tatu kwa upande wa Swansea lilimaliza matumaini ya Liverpool japo kuondoka na pointi moja kutoka uwanja wa ugenini.
Brad Smith kwa upane wa Liverpool alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuoneshwa kadi mbili za njano.
Matumaini ya Liverpool kufuzu kucheza Champions League yamebaki kuwa ni kutwaa taji la Europa League pekee.
Ushindi huo unamaana kubwa kwaSwansea ambao wamebakiza michezo miwili tu kabla ya ligi kumalizika, matokeo hayo yanawafanya wasalie nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi huku wakiweka gap la pointi 11 kati yao na Sunderland inayoshika nafasi ya tatu kutoka chini.
Mambo muhimu ya kufahamu
- Andre Ayew amefunga magoli mawili kwenye mechi moja kwa mara ya kwanza tangu atue Swansea.
- Swansea imefurahia ushindi wake wanne mfululizo kwenye uwanja wa nyumbani, ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwenye Premier League.
- Christian Benteke amefunga goli lake la 50 ndani ya Premier League.
- Swansea imefunga magoli matatu kwenye Premier League kwa mara ya kwanza tangu ilipofanya hivyo mara ya mwisho 25 April, 2015, time Jack Cork kwa mara ya mwisho.
- Gylfi Sigurdssonamehusika kwenye magoli 41 ya Swansea ndani ya Premier League (amefunga magoli 25 na kutoa assists 16), magoli 10 zaidi ya mchezaji yeyote wa Swansea (Wilfried Bony ndiye anayefata akiwa kahusika kwenye magoli 31 wakati akiitumika klabu hiyo).