Licha ya Yanga kupata ushindi kwenye mchezo wake wa kimataifa wa kombe la shirikisho barani Africa dhidi ya Esparanca ya Angola, kuna baaddi ya watu wamekuwa wakise, kukosekana kwa wachezaji wawili wa kimataifa kutoka Zimbabwe Donald Ngoma na Thabani Kamusoko kumeifanya Yanga kupwaya na kuhangaika kiuchezaji.
Kocha wa Yanga Hans van Pluijm anasema timu yake haitegemei mchezaji mmoja-mmoja, badala yake ameijenga timu kucheza bila kuwepo kwa mchezaji yeyote ndiyomaana hata walipokosekana wachezaji hao bado timu ilicheza na kupata ushindi.
“Timu siyo Ngoma, sijawahi kumleta mchezaji mmoja mbele ya watu kwasababu mchezo wa soka unategemea timu nzima. Kama ngoma ataumia na kupata majeraha inamaana timu isicheze?”, alihoji Hans wakati anajibu swali aliloulizwa kwenye mkutano na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Yanga na Esparanca.
“Na kama hakuwepo kwenye mchezo unatakiwa kuwa na plan nyingine ya kucheza bila yeye, na tulifanya hivyo, tulitengeneza nafasi nyingi na hatimaye tukapata ushindi.”
“Nikiwa kama kocha, natakiwa natakiwa kuwajengea wachezaji kujiamini na kucheza bila mchezaji yeyote kuwepo uwanjani kwasababu kama utaijenga timu kwa kumtegemea mtu mmoja iposiku akikosekana wachezaji watapata wakati mgumu uwanjani.”
Yanga iliwakosa Noma na kamusoko kutokana na wachezaji hao kutumikia kadi tatu za njano kwenye michuano ya kimataifa, lakini watakuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza mchezo wa marudiano huko Angola.