Savio Basketball Club inayotokea Upanga Don Bosco jijini Dar es Salaam imechukua ubingwa wa taifa baada ya kuifunga timu ya jeshi ya ABC kwa vikapu 77 kwa 66 kwenye fainali iliyofanyika Jumapili ya tarehe 15 ndani ya uwanja wa taifa wa (Basketball Indoor Stadium).
Amini Mntambo ndiyo mchezaji bora wa hii ligi kutoka Savio mwenye jezi number 14 mgongoni, Michuani hii ilianza tarehe 7.5.2016 na jana Jumapili ndiyo ilikuwa kilele chake.
Savio kwa mara ya kwanza walishiriki mashindano haya mwaka 2005 yaliyofanyika tanga ambapo fainali walikutana na timu ya jeshi ya JKT na kuwafunga, Savio kupitia ligi hii ya taifa wameshachukua ubingwa huu zaidi ya mara 5, walichukua ubingwa miaka mitatu mfululizo mwaka 2009/2010, 2010/2011, 2011/2012.
Savio imefuzu kucheza zone 5 na kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Afrika Mashariki na Kati yatakayofanyika mwanzoni mwa mwez wa nane.