FA Cup ndiyo kombe la zamani zaidi duniani, kwa mara ya kwanza lilianzishwa msimu wa 1871-72, likihusisha vilabu vyote vya England (Premier League, Football League na hata vilabu ambavyo haviko kwenye ligi).
Arsenal ndiyo klabu iliyotwaa mara nyingi zaidi kombe la FA, ikiwa na rekodi ya kutwaa taji hilo mara 12 ikifuatiwa na Manchester United iliyochukua mara 11 huku Tottenham Hotspur wao wakiwa wamelibeba mara nane.
Wakati Manchester United wakitarajia kupambana na Crystal Palace kwenye mchezo wa fainali ya FA Cup leo jioni kwenye uwanja wa Wembley huku ndoto zao zikiwa ni kushinda taji hilo na kuifikia rekodi ya Arsenal kama timu yenye mafanikio kwa upande wa FA Cup, hii ni orodha ya washindi wa FA Cup tangu lilipoanzishwa mwaka 1871.
12 titles: Arsenal
11 titles: Manchester United
8 titles: Tottenham Hotspur
7 titles: Liverpool, Chelsea, Aston Villa
6 titles: Newcastle United, Blackburn Rovers
5 titles: Everton, West Bromwich Albion, Manchester City, The Wanderers
4 titles: Wolverhampton Wanderers, Bolton Wanderers, Sheffield United
3 titles: Sheffield Wednesday, West Ham United
2 titles: Preston North End, Old Etonians, Portsmouth, Sunderland, Nottingham Forest, Bury
1 title: Wigan Athletic, Huddersfield Town, Southampton, Leeds United, Derby County, Royal Engineers, Oxford University, Blackpool, Cardiff City, Burnley, Charlton Athletic, Barnsley, Notts County, Clapham Rovers, Wimbledon, Coventry City, Ipswich Town, Bradford City, Blackburn Olympic, Old Carthusians.