Mgogoro wa unaoendelea katika klabu ya Stand United umechukua sura mpya baada ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga kuuvunja uongozi wa klabu hiyo na kutanga uongozi wa mpito.
Ungozi wa Stand United umepinga maamuzi hayo ukidai kwamba, Mkuu wa Wilaya hana mamlaka kisheria kuvunja uongozi wa klabu yeyote iliyomwanachama wa TFF kwasababu kiongozi huyo si mwakilishi wa TFF, CAF wala FIFA.
Tangu klabu hiyo ipate udhamini kutoka kampuni ya uchimbaji madini ya ACACIA kumekuwa na migogoro ndani ya timu hiyo ambayo imekuwa ikiiathiri hadi timu kwenye matokeo ya uwanjani.
Mwenyekiti wa klabu ya Stand United Aman Vicent amemuandikia barua katibu mkuu wa TFF Bw. Mwesigwa Selestine huku nakala za barua hiyo zikienda kwa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Michezo, Katibu Mkuu Baraza la Michezo, Msajili vyama vya Michezo na SHIREFA kwa taarifa.
Kwa taarifa zaidi, hii hapa barua iliyoandikwa na Mwenyekiti wa Stand United kwenda kwa Katibu Mkuu wa TFF.