Zimebaki saa chache kabla ya kushuhudia fainali ya vilabu bingwa Ulaya ikipigwa kwenye uwanja wa San Siro, Milan Italy kati ya miamba miwili ya soka la Hispania Real Madrid vs Atletico Madrid ambayo pia inatoka katika jiji moja la Madrid.
Katika pitapita zangu za hapa na pale wakati nikisubiri muda ufike ili nijisogeze uwanjani, nikaona si vibaya kama nitakupa hali halisi ya mambo ilivyo nje ya uwanja.
Mashabiki ni wengi na pilika ni nyingi kila mtu akiwa yuko tayari kuishudia timu yake ikipambana kutafuta ubingwa wa Ulaya kwa ngazi ya vilabu.
Dondoka na picha hizi….