Michuano ya Sports Extra Ndondo Cup chini ya udhamini wa Dr. Mwaka imeendelea tena leo, kwenye uwanja wa Bandari ulipigwa mchezo kati ya Stakh Shari vs Keko Furniture.

Mchezo huo umemalizika kwa Keko Furniture kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ambalo lilifungwa na Meshack Abel kipindi cha kwanza na kudumu kwa dakika zote za mchezo huo.
Ukiachana na ndani ya uwanja, kama kawaida ya Ndondo Cup nje ya uwanja huwa ni burudani kutoka kwa vimundi vya ushangaliaji ambavyo huwa vinazi-support timu zao mwanzo mwisho wakati zinapambana uwanjani.

Mashabiki wa Keko Furniture ndiyo walifunika kwa upande wa leo kutokana na kuishangilia timu yao kwa dakika zote 90 za mchezo huku wakitumia style mbalimbali kutoa burudani hiyo.

