Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

EXCLUSIVE: SIMBA WALISHINDWA KUFIKIA DAU, YANGA WAKAMALIZA MCHEZO-KAKOLANYA

$
0
0

Kakolanya

Siku chache baada ya kusajiliwa na mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara klabu ya Yanga, golikipa Beno Kakolanya amepiga story na shaffihdauda.com kuhusu mambo mbalimbali ambayo mengine inawezekana ulikuwa huyajui kuhusu golikipa huyu aliyetamba na Tanzania Prisons ya Mbeya na kuisaidia kumaliza katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.

Ungana na Yahaya Mohamed ambaye alipata fursa ya kuzungumza na Kakolanya aliyejiunga na kikosi cha Jangwani.

Beno Kakolanya: Nimepokea kwa furaha kwasababu naenda kukutana na watu wazoefu na waliocheza kwa muda mrefu, kuna golikipa kama Deo na Barthez. Kuna watu wananiambia unaenda pale lazima nikakae benchi, lakini hayo ni maneno tu, kwangu mimi naona naenda kupata changamoto kubwa kwasababu wao ni wazoefu, wao watacheza lakini mimi nitakapopewa nafasi nitaitumia zaidi.

www.shaffihdauda.co.tz: Mwanzo kwenye vyombo vya habari ilitajwa kwamba, ulikuwa unaelekea kusajiliwa na Simba, lakini ghafla umetangazwa umesajiliwa na Yanga. Kitu gani kilitokea hapo katikati?

Beno Kakolanya: Mazungumzo na maelewano tu, maana wao wameshindwa lakini Yanga wamekuja tumeongea tumeelewana, dau nililotaka wamenipa nikasaini. Na nimeenda pale kwa sababu kubwa, watu wanafanya kazi.

www.shaffihdauda.co.tz: Mchakato wako wa uhamisho ulikuwaje kwa maana ya mawasiliano mpaka hatua ya mwisho dili likakamilika?

Beno Kakolanya: Tangu ligi inakaribia kuisha mwezi mzima Yanga walikuwa wananifatilia lakini ligi ilipoisha, Prisons walihitaji nibaki nikawaambia tutaongea baada ya kutoka timu ya taifa. Nimeenda kule dau nililokuwa nalitaka mimi wao walikuwa hawana, Yanga wakaja na dau ambalo nalihitaji mimi nikaenda.

www.shaffihdauda.co.tz: Umekaa Tanzania Pisons kwa muda gani?

Beno Kakolanya: Msimu ulioisha ni mwaka wa tatu.

www.shaffihdauda.co.tz: Watanzania wengi hususan wapenzi wa Yanga wangependa kujua historia yako katika mpira kwa ufupi  umezaliwa wapi na umeanzia wapi kucheza soka?

Beno Kakolanya: Nimezaliwa Sumbawanga, baba na mama walikuwa ni askari. Nimemaliza darasa la saba Sumbawanga na nikaanza form one palepale. Mpira nimeanza kucheza baada ya kumaliza darasa la saba, nikiwa kama beki na baadaye striker halafu nikahamia kuwa golikipa.

Kulikuwa na kocha wangu alikuwa na timu inaitwa Sinza maeneo ya Kantalamba Sekondari, yule ndiyo alikuwa mtu wa kwanza kuniona na akaniambia nijiunge nae kwasababu anaona ninaweza. Nilikuwa dogo wakati huo nikawa naogopa kucheza na watu wazima.

www.shaffihdauda.co.tz: Kipi kilikuhamisha kutoka nafasi za ndani ulizokuwa unacheza awali na kukurudisha kuwa golikipa?

Beno Kakolanya: Nilienda Mbeya kwa babu yangu, sasa alikuwa na wajukuu wengi sana. Siku moja tukakusanyana wajukuu wengi tukaenda kijiji kingine kucheza mechi. Tukiwa kule tukawa hatuna golikipa nikaambiwa mimi nikae golini.

Nilikaa golini lakini nilikuwa situmii mikono, nacheza kwa kutumia miguu. Nilivyorudi Sumbawanga nikaona naweza, nikawa nacheza golini na ndani mwisho wa siku golini kumenifit lakini ukiniweka ndani nacheza kama kawaidia.

www.shaffihdauda.co.tz: Kuna golikipa yeyote anayekuvutia na kukufanya wewe uwe bora kama ulivyo hivi sasa?

Beno Kakolanya: Golikipa anayenivutia zaidi ni Juma Kaseja, napenda sana jinsi anavyocheza lakini nataka nifanye zaidi yake yeye.

www.shaffihdauda.co.tz: Baada ya kuitwa timu ya taifa na kufanya mazoezi kwa muda, umesikika ukisifia mazoezi ambayo ulikuwa ukipewa na kocha wa makipa wa timu ya taifa Peter Manyika. Kipi cha ziada ambacho umekutana nacho huko ambacho hukuwahi kukutana nacho?

Beno Kakolanya: Golikipa anamazoezi mengi, lakini kikubwa golikipa mazoezi yake makubwa ni stapping golini. Sasa nimeenda pale nimekuta mazoezi mengi ndiyo yale ambayo kwa asilimia kubwa sijayafanya ndiyo yamenivutia na kuniongezea kitu cha ziada.

www.shaffihdauda.co.tz: Namba 30 ya jezi ambayo unaivaa inamaana yoyote kwako maana tumezoea kuona magolikipa wanavaa jezi namba 1.

Beno Kakolanya: Jezi namaba 30 siyo jezi ninayoipenda, namba ninayoipenda mimi ni namba 25 lakini nimekuja hapa nikaiomba lakini ikawa imetolewa kwa mchezaji wa ndani, ikabidi nichukue namba 30. Naipenda tu kutoka moyoni lakini haina maana yeyote.

www.shaffihdauda.co.tz: Kuna washambuliaji ambao huwa unawaogopa pindi unapocheza na timu zao?

Beno Kakolanya: Kuna wachezaji kama Ajib, Ngoma, Tambwe, hao wanauwezo na wanasumbua ukichezanao lazima ufanye kazi ya ziada.

www.shaffihdauda.co.tz: Wachezaji wanaotoka mikoani kuja Dar, huwa wanapotea kwasababu ya vitu ambavyo wanakutana navyo kama vile starehe na mambo mengine. Umejiandaa vipi kukabiliana na hali hiyo na kulinda kiwango chako kiendelee kusimama kama kilivyo?

Beno Kakolanya: Mimi nimejiandaa vizuri, unajua ni kujitambua mwenyewe. Watu wengine wakifika Dar wanaona ndiyo wamefika, lakini maisha ni safari ndefu nyumbani kuna watu wengi wanakutegemea kwa hiyo ukitambua unachokifanya lazima mambo yatanyooka.

www.shaffihdauda.co.tz: Ni mechi gani unayoikumbuka kati ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ambayo huwa inakuumiza sana au inakufurahisha sana

Beno Kakolanya: Mechi yetu na Simba msimu huu uliomalizika, ile mechi tumefanya kazi kubwa sana hadi wao walikuwa hawaamini, dakika za mwisho wakafunga goli. Siwezi kuisahau ile mechi hadi mashabiki wao walianza kutoka nje lakini baadaye wakarudi ndani kuja kushangilia goli.

www.shaffihdauda.co.tz: Kwenye upande wa muziki ni msanii gani anakuvutia kiasi kwamba muda mwingi unakaa na kusikiliza ngoma zake?

Beno Kakolanya: Msanii anayenivutia ni Ali Kiba kwasababu anasauti nzuri na anaimba vizuri, japo kuna ushindani na watu wangine wanasema hana kitu lakini kuna vitu vingine inabidi tuwe wakweli.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles