Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

MTIBWA SUGAR YATHIBITISHA KUPOKEA OFA NYINGI KUTOKA…

$
0
0

Yanga-vs-Mtibwa-znz-3

Na Baraka Mbolembole

Mtibwa Sugar ya Turiani, Morogoro kupitia kwa msemaji wake Thobias Kifaru imesema kwamba imepokea ofa nyingi kutoka klabu za Azam FC na Simba SC zikiwahitaji wachezaji wake ambao kwa kiasi kikubwa walionesha viwango vikubwa ndani ya uwanja msimu uliopita.

“Kundi kubwa la wachezaji wetu wanatakiwa na na klabu za Azam na Simba. Siwezi kutaja majina ya wachezaji ambao ofa zao zimetufikia lakini ni kundi kubwa sana”, anasema Kifaru.

Mlinzi wa kati na naodha msaidizi, Salim Mbonde amemaliza mkataba wake lakini tayari aliiambia www.shaffihdauda.co.tz kwamba hatojiunga na timu yoyote kubwa nchini na badala yake atajifunga tena kwa mwaka mmoja zaidi katika timu hiyo aliyoichezea kwa misimu mitatu iliyopita.

Mbonde ataenda nje ya nchi kujaribu kucheza soka la kulipwa na ikiwa atafanikiwa inamaanisha kuwa Mtibwa haitakuwa na walinzi wake wote wa kati msimu ujao kufuatia Vicent Andrew kusaini mkataba wa miaka miwili kwa mabingwa Yanga SC.

Mchezaji wa nafasi ya kiungo, Mudhamir Yasin, wing Shiza Kichuya, mlinzi wa pembeni Ally Shomari wote wanatakiwa na klabu hizo za Dar es Salaam ambazo zilimaliza katika nafasi za pili (Azam FC) na ile ya Tatu ( Simba SC) msimu uliopita.

“Tumecheza kwa mafanikio makubwa kwa miaka 21 sasa katika ligi kuu ya soka Tanzania Bara, niseme kwamba jambo kubwa linalofanya klabu hii iweze kutengeneza nyota wengi wa uhakika ni kutokana na uongozi bora uliopo katika mfumo wa kampuni.”

“Tumekuwa tukiwalea vizuri wachezaji wetu vijana. Mtibwa ni chuo kizuri ambacho kimekuwa kikizalisha vipaji vingi katika sola la Tanzania na tutaendelea kufanya hivyo kutoka na misingi mizuri tuliyoijenga. Tunafurahi kuzalisha vipaji bora ambavyo vimekuwa lulu, ila klabu zifuate taratibu za usajili zinazokubaliwa”, anasema Kifaru.

Said Bahanunzi, Juma Abdul, Shaaban Kado, Hussein Javu ni baadhi ya nyota waliowahi kusajiliwa na Yanga miaka ya karibuni baada ya kufanya vizuri Mtibwa.

Shaaban Nditti, Musa Hassan Mgosi, Abdulhalim Humud, Hussein Shariff, Issa Rashid, Paul Ngalema hawa ni baadhi ya waliopata kusaini Simba nyakati tofauti wakitokea Mtibwa Sugar.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>