Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

MIRAJ ADAM ‘MR. FREEKICK’ : NIPO TAYARI KUICHEZEA TIMU YOYOTE ISIPOKUWA…

$
0
0

Miraji Adam

Na Baraka Mbolembole

“Sijajua kama nitarejea Simba maana viongozi bado hawaeleweki,” anasema mlinzi wa pembeni na ‘mtaalamu wa mipira iliyokufa,’ Miraj Adam katika moja ya majibu yale ya wazi kwa mashabiki wake waliomuuliza kama atarejea kuichezea Simba SC, timu mkataba wake unaelekea ukingoni.

Miraj ameichezea Simba kwa miaka mitano akitokea timu ya vijana ya klabu hiyo ambayo imewahi kumtoa kwa mkopo katika timu za Mtibwa Sugar (2014/15 wakati wa mzunguko wa pili) na Coastal Union ya Tanga wakati wa mzunguko wa pili msimu uliopita.

“Mkataba wangu na Simba unaelekea ukingoni na nitakuwa tayari kuichezea timu yoyote isipokuwa ya ligi daraja la kwanza. Malengo yangu ni kucheza mpira wa kulipwa siku za mbeleni hivyo nikicheza ligi daraja la kwanza nahisi nitachelewa. Nitaichezea tena Simba wakija na kufanya mazungumzo, tukielewana nitarejea kwa sababu mpira ni kazi yangu.”

Anasema mlinzi huyo wa pembeni ambaye anakumbukwa kwa magoli yake ya faulo wakati Coastal ilipozishinda Yanga SC na Azam FC katika michezo ya VPL msimu uliopita.

Simba ilimsaini Miraj akitokea timu B ya Azam FC na mchezaji huyo anasema alihitaji kuwahi kucheza ligi ya juu ili kutimiza malengo yake.

“Nilipokuwa Azam B wakati huo kulikuwa hakuna mipango ya mchezaji kutoka kikosi cha pili kwenda timu ya kwanza, kubaki pale niliona ni sawa na kujichelewesha ndiyo maana nikasajili Simba.” Tangu alipoanza kuichezea timu ya kwanza ya Simba msimu wa 2012/13, Miraj amekuwa akiandamwa na balaa la majeraha.

“Matatizo ya maumivu kidogo yameniathiri ndiyo maana nilishindwa kucheza vizuri. Nilikuwa na uoga wa kuumia kila nilipokuwa uwanjani, ila sasa namshukuru Mungu nipo vizuri ndiyo maana nilifanya vizuri nilipokuwa Coastal. Mungu akinipa afya nitafanya vizuri zaidi.”


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>