Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

KAMUSOKO AMEANDIKA UJUMBE MZURI KUM-WISH MKEWE HAPPY BIRTHDAY

$
0
0
Ujumbe wa Kamusoko kum-wish mkewake happy birthday uliambata na picha hii
Ujumbe wa Kamusoko kum-wish mkewake happy birthday uliambata na picha hii

Leo Julai 26 mke wa kiungo wa Yanga Thaban Kamusoko anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa (birthday), katika kuona umuhimu huo, mumewake (Kamusoko) ameandika ujumbe kwenye account yake ya facebook akimtakia kila la heri mkewake kipenzi.

Kamusoko ambaye leo atakuwa akiiwakilisha klabu yake Yanga kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Medeama mchezo unaopigwa nchini Ghana.

Ujumbe wa Mzimbabwe huyo ambaye ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa kigeni unasomeka hivi: “Wana take this opportunity to wish my wife a happy birthday and may the lord grant her with more happiness and more blessings…..im happy to have you in my life…..will always love you ‪#‎Bongile Sibanda,” ujumbe huo mzuri ndivyo ulivyomalizika.

Kiungo huyo wa Jangwani amekua akionekana mara kadhaa na mkewe pamoja na motto wao mdogo kwenye matukio makubwa yanayoihusu klabu ya Yanga. Walikuwa pamoja siku Yanga ikikabidhiwa ubingwa wa VPL pamoja na FC Cup lakini pia walikuwa pamoja kwenye utoaji tuzo kwa timu, wachezaji na makocha kwa ajili ya msimu uliopita wa ligi kuu Tanzania bara.

shaffihdauda.co.tz inaungana na Thaban Kamusoko kumtakia mkewe maadhimisho mema ya siku yake ya kuzaliwa.

Happy birthday Mrs. Kamusoko.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>