Mchezo wa kirafiki kati ya Simba dhidi ya Polisi Moro umepigwa katika uwanja wa chuo cha High Land uliopo Bigwa nje kidogo ya manispaa ya Morogoro mjini
Mchezo huo umemalizika kwa Simba kupata ushindi wa bao 6-0 dhid ya maafande wa Polisi Moro.
Mabao ya Simba yamefungwa na Fredric Blagnon aliyefunga dakika ya 5 na dakika ya 16 kipinda cha kwanza.
Magoli ya mengine ya Simba yamefungwa kipind cha pili, Ibrahim Ajibu alifunga mara mbili katika dakika ya 48 na 73 bao la tano limewekwa wavuni na Abdi Banda dakika ya 82 huku Mohamed Musa “kijiko” akihitimisha ushindi huo kwa goli la sita dakika ya 86.