Timu ya soka ya Lyon ya nchini Ufaransa imekataa ofa ya euro mil 35 (paundi 29.3m) kutoka kwa klabu ya Arsenal kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wao Mfaransa Alexandre Lacazette.
Lacazette (25) alifunga mabao 21 kwenye mechi za ligi 34 msimu uliopita na bado ana mkataba na timu hiyo mpaka mwaka 2019.
Katika taarifa iliyoyotolewa kwenye ukurasa wa Twitter wa klabu hiyo inaeleza kwamba “Lacazette ni mchezaji ambaye pengo lake si rahisi kuzibika na ni moja ya viongozi wazuri kwenye timu chini ya kocha Bruno Genesio.”
Lyon imekanusha taarifa za vyombo vya habari zinazoeleza kwamba wamekataa ofa ya euro mil 48 (paundi mil 42.2) kutoka kwa washika bunduki hao wa London.