Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

NYOSSO ATAKUMBWA NA ADHABU HII…

$
0
0
NYOSO
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
WAKATI Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) itakaa muda wowote kutoa adhabu dhidi ya beki wa kati Juma Nyosso, nahodha huyo wa Mbeya City yuko hatarini kufungiwa miaka miwili kucheza soka kutokana na kurudia tabia yake chafu ya kuwashika sehemu za makalio wachezaji wa timu pinzani.
Rais wa TFF alisema juzi kuwa tukio hilo wameliona na watachukua hatua ya kumwadhibu mchezaji huyo wa zamani wa Simba ambaye amekuwa gumzo kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii baada ya Jumapili kumdhalilisha kwa mtindo huo nahodha wa Azam FC.

Kwa mujibu wa Kanuni za Ligi za TFF, Nyosso yuko hatarini kufungiwa kusakata soka rasmi kwa kipindi cha miaka miwili kutokana na kumdhalilisha mkali huyo wa mabao (Bocco).
 
KANUNI ZA TFF
Kanuni ya 37 Kifungu cha 24 cha Kanuni za Ligi za TFF toleo la 2015 kinasema: “Mchezaji yeyote atakayepatikana na hatia ya kufanya makosa makubwa ya kimaadili au kinidhamu, au ya kibaguzi au ya kidhalilishaji au yatakayotafsiriwa kuwa ni ukiukaji mkubwa wa taratibu za mchezo na ubinaadamu atatozwa faini kati ya shilingi milioni moja mpaka milioni tatu au/na kusimamishwa kushiriki michezo mitatu mpaka kumi ya klabu yake yoyote atakayoitumikia katika Ligi Kuu na mashindano mengine rasmi ya TFF au kufungiwa kipindi cha kati ya mwaka mmoja na miwili.”

Hii si mara ya kwanza mchezaji huyo wa zamani wa Simba (Nyosso) kufanya kitendo hicho kwani Februari 28 mwaka huu alitenda kadhia hiyo, kosa ambalo lilipelekea kufungiwa mechi nane na TFF. Nyosso pia aliwahi kuwadhalilisha kwa mtindo huo nyota kadhaa wa Tanzania wakiwamo, Amir Maftah na Joseph Kaniki.

Kanuni ligi kuu

Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>