Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

MAFANIKIO YA LA MASIA BAADA YA FC BARCELONA KUNUNULIWA 1954, MO ATAFUATA…?

$
0
0

IMG_0344

Na Baraka Mbolembole

Baada ya uongozi wa Simba SC kufungua mazungumzo rasmi na tajiri Mohammed Dewji kuelekea mpango wa mabadiliko-kutoka mfumo wa kadi hadi Simba kampuni wengi wamekuwa na shauku ya kutaka kuona timu hiyo ikirejea katika makali yake ndani ya uwanja na kupiga hatua kiuwekezaji na kiuchumi baada ya miaka 80 ya ‘kutaabika.’

Kikubwa ambacho kimeifanya FC Barcelona kuwa miongozi mwa timu vigogo barani Ulaya ni La Masia-Shule yao ya soka. Mataji yao matano ya ligi ya mabingwa yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na vijana waliozalishwa na kukuzwa La Masia.

Mpango kama huu unaweza kutengeneza timu bora ya muda mrefu lakini unahitaji uwekezaji mkubwa, subira na uvumilivu. Kwa timu kubwa kama Simba mpango huu ni jambo la lazima na pengine mabadiliko tarajiwa yanaweza kumfanya MO kuiga mpango huu wa La Masia na pale Bunju wakazalishwa kina Leo Messi wetu.

Tafadhali soma hapa kujua namna kina Messi, Xavi, Iniesta, Busquets wanavyozalishwa.

La Masia….

Mwaka 1979 Johan Cruffy alitaka kuuanzisha taasisi kivuli ya Ajax ndani ya Barcelona. Ombi lake lilikubaliwa na Rais Josep  Nunez. La Masia ina makazi  ya kizamani  yaliyojengwa mnamo mwaka 1702,  kabla ya Barcelona kununuliwa mnamo mwaka 1954.

Klabu ilikuwa tayari kuitumia La Masia kama soko kwa madhumuni ya kujenga uwanja mpya Camp Nou (wa sasa)  baada ya Camp Nou  ulioanzishwa mnamo 24, septemba, 1957.

La Masia ilifungwa na kufanyiwa matengezo upya chini ya aliyekuwa  rais wa klabu hiyo, Enric Llaudet, na likajengwa jengo kubwa na la kisasa ambalo lilifunguliwa mnamo 26 Septemba, 1966 (miaka tisa baada ya kuvunjwa kwa matengenezo mapya).

La Masia mwanzoni haikuwa na  nafasi ya kuajiri wafanyakazi wengi kwani klabu ilikuwa inaendelea kukua taratibu na aliyekuwa  rais Josep Nunez alitaka kubadili mfumo mnamo 1979 wa nyumba ya vijana ya Taasisi hiyo ya Barcelona.

Wazo la Taasisi hiyo lianzishwa na Núñez  na Johan Cruffy mchezaji wa zamani wa timu hiyo na rais wa maisha wa klabu hiyo ya Catalunya ambaye alikuwa zao la Taasisi ya Ajax (Ajax Academy.) Núñez yeye alipendekeza eneo na vifaa ‘Oriol Tort’ na  alikuwa msimamizi wa shughuli zote za ujenzi.

Mmoja kati ya zao la Taasisi hiyo ni kiungo  Guillermo Amor  ambaye alikuwa na uwezo wa juu  ilikuwa ni mwaka 1988. Amor alicheza jumla ya mechi 311 za ligi ya Hispania La Liga katika kikosi cha kwanza.

Miaka miwili baadae  alifuatiwa na golikipa Carles Busquets na kiungo Josep Guardiola ambaye alikuwa kocha wa timu hiyo kati ya 2008-2012. Wote watatu walikuwa wanaunda kikosi cha kwanza  chini ya Cruyff, ambaye alikuwa meneja wa timu mwaka 1988.

Timu ya Cruyff ilicheza kimpangilio kutokana na ‘philosofia’ ya  timu kucheza vizuri (total football) ambapo imekuwa ndio utaratibu wao  ndani ya Barcelona mpaka kufikia mafanikio walio nayo.

Guardiola kutokana na uwezo wake wa nafasi ya kiungo amekuwa mzalishaji mzuri wa viungo kutoka La Masia kama vile Xavi Hernandez, Andres Iniesta na Cesc Fabregas na Sergio Busquets.

Kwa kipindi hiki cha miaka 8,  Xavi ndie ameonekana kufuata nyayo za Guardiola katika nafasi ya kiungo na kufuata sheria zote za kiungo.

Guardiola aliteuliwa kukinoa kikosi cha pili  cha Barcelona May 2007 kwa kipindi hicho timu ilikuwepo na ikaweza ikaingia kwenye ligi daraja la  nne nchini Hispania.

Kutokana na uwezo wa timu B ikaanzishwa Barcelona C ambayo ilicheza kwenye ligi hiyo. Guardiola aliamua  Barcelona B kuchanganyika na timu ya vijana chini ya umri wa miaka  21 kwa dhumuni la kuleta upinzani na kuwakomaza wakati wakiwa kwenye ligi.

Aliigawa timu katika makundi mawili ambayo alijumuisha vijana wadogo na wale kati ya miaka 21-26 wa kikosi B walikuwa wanakaa kwa miaka miwili kabla ya kuuzwa.

Kwa upande mwingine Guordiola alimtaka aliyekuwa rais wa timu hiyo Joan Laporta kuongeza vifaa vingine vizuri kwa lengo la kufundishia ili timu iweze kwenda  Ciutat Esportiva Joan Gamper  ambapo Laporta ana maabara yenye vifaa vya kutosha sehemu ambayo itamsaidia kocha kufundishia kwa umakini.

Mwishoni mwa msimu wa  2007-2008, Barcelona B iliweza kushika nafasi ya tatu  katika ligi ya Segunda B na mwishoni mwa mwaka 2009-2010 wakamaliza katika nafasi ya pili, ambayo ni nafasi ya juu katika wachezaji wa akiba wa kikosi cha kwanza kinachocheza ligi kuu  (Primera Division).

La Masia inaripotiwa sana hivi sasa baada ya Barcelona B kufanikiwa , Mmoja wa wachezaji walioozalishwa  hapo, Rory Smith aliwahi kusema:“La Masia ni mbadala wa Ajax Academy kwa uzalishaji wa wachezaji” Mafanikio ya La Masia ni kutokana na shule ya vipaji kama Cesc Fabregas, Lionel Messi, Gerald Pique, Pedro Rodriguez, Sergio Busquets. Thiago Alcantara, Bojan Krick, Giovann Dos Santos, Victor Valdes, na wengineo.

Mwaka 2000, Louis Van Gaal akiwa kocha wa FC Barcelona alikaririwa na vyombo vya habari vya michezo kwamba ndoto zake ni kushinda taji la klabu bingwa Ulaya akiwa na wachezaji 11 wazawa, lakini alishindwa kutokana na kuwakumbatia sana wachezji wa Kiholanzi.

Timu ya kwanza iliyowahi kushinda michuano hii ilikuwa na wachezaji nane wazawa mnamo mwaka 2009, tena ikiwa chini ya Pep. Ni zaidi ya miaka 30  tangu kuanzishwa kwa taasisi  hii ya La Masia,  na ina jumla ya vijana wadogo 500 ambao wametoka majumbani kwao kwenda kuishi kwenye taasisi.

Nusu yao wametoka Catalunya na wengine wametoka sehemu mbalimbali katika mikoa ya falme za Hispania na waliobaki ni 15 kutoka Cameroon, saba Brazil,  watano kutoka  Senegal na  watatu kutoka Argentina na hao kati ya 500 ni asilimia kumi wanaunda kikosi cha kwanza.

Kila kitu Kwa umoja

Timu ya Barcelona huchea kuanzia mwezi Agosti hadi Mei.  Kwa baridi huko La Masia sababu inayopelekea timu kucheza mwaka mzima na wachezaji wa kikosi B na C wanajifunza baada ya kutoka shule wakati wa jioni na asubuhi na wanafundishwa na wachezaji wa zamani wa FC Barcelona.

Timu ya  Barcelona B inakuwa  na walimu 24 na zaidi ya wachezaji 300. 56 wameajiriwa wakiwemo madaktari wapishi na wengineo katika kipindi cha msimu wa  mwaka 2009-10 timu B ilifanikiwa kuingia Segunda Division kwa mara nyingine.

Barcelona B inacheza mfumo wa kama unaotumika kwenye timu ya wakubwa 4-3-3. Hiyo imefanya kuwa na mafanikio katika kipindi cha miaka sita iliyopita katika michuano ya Ulaya.

Sergio Busquets ni mmoja kati ya zao la La Masia ambaye mmojwapo kati ya wachezaji wakikosi cha kwanza cha Barcelona tangu 2008 hadi sasa na tayari ana rekodi ya kucheza michezo zaidi ya 300 na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji kijana zaidi kucheza michezo mingi ndani ya klabu hiyo.

Kwenye chumba cha kulia chakula cha La Masia  kuna  saini zimepigwa kwa lugha ya  Catalan kwa ajili ya kuwahamasisha wachezaji chipukizi kujituma na kujitolea na kweli wanafanya hivyo. Saini kama za nyota waliopita wa klabu hiyo kama Pep.

“Kila mchezaji anayepitia La Masia  anakuwa na kitu fulani tofauti,na wanaokuja  kuvaa jezi za Barcelona toka wakiwa wadogo,” aliwahi kusema Pep.

“Wachezaji wote wa Catalunya lazima wapitie La Masia kwani shule hii huzalisha aina bora ya soka Duniani-mfano mzuri ni Sergio Busquets ambaye ni kiungo bora katika pasi za one-two na ni kinda mwenye rekodi za ajabu kutoka La Masia. La Masia ni chuo bora zaidi ya kile cha Ajax Amsterdam ambacho kiliwaibua nyota kama  Johan Cruffy”  aliwahi kusema  Xavi Hernandez.

Dairekta wa zamani wa  benchi la ufundi,  Pep Segura, aliweza kuleta mafanikio ‘kwa aina ya uchezaji’  kiakili kutoka chini mpaka kuwa juu katika timu  ya  Barcelona  wanaendelea kupata mafanikio kutokana na uchezaji wa kupiga pasi  nyingi.

Kwa ukaribu zaidi, tafadhali unaweza ku-LIKE PAGE yangu #BSports. Utapata Updates za michuano…..


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>