Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

UTHIBITISHO WAPATIKANA KAMA MWINYI ANATUMIA AU HATUMII MADAWA YA KULEVYA 

$
0
0

Mchezaji Mwinyi Haji

Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar

Baada ya kuzagaa picha mbalimbali na taarifa kuwa mlinzi wa kushoto wa Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania Mwinyi Haji Ngwali ‘Bagawai’ anatumia madawa ya kulevya, taarifa hizo si kweli na wala mlinzi huyo wa kushoto wa Yanga hatumii madawa yoyote kama inavyodaiwa.

Mwinyi Haji Ngwali hatumii dawa za kulevya na uthibitisho huo umetolewa na Awattif A. Abdulrasoul ambae yeye ni Mkemia Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Tarehe 09/05/2016 Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ilipokea test tube moja ya damu na kikopo kimoja cha mkojo wa Mwinyi Haji kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kitaalam.

Uchunguzi ulifanyika kwa kutumia (Diffusion Assay Method na mult-line screen device test) umethibitisha kutokuwepo kwa ulevi ndani ya damu na aina yoyote ya madawa ya kulevya ndani ya mkojo.

Uthibitisho kutoka kwa Mkemia mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar uliobaini kwamba, kwenye damu na mkojo wa Mwinyi hakukuwa na aina yoyote ya chembechembe za madawa ya kulevya
Uthibitisho kutoka kwa Mkemia mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar uliobaini kwamba, kwenye damu na mkojo wa Mwinyi hakukuwa na aina yoyote ya chembechembe za madawa ya kulevya

Haji Ngwali ambae ni baba mzazi na wakala wa Mwinyi amethibitisha kuwa mtoto wake hatumii madawa hayo na ili kuthibitisha hilo, alimpeleka kwa Mkemia mkuu wa Zanzibar na amethibitisha kuwa Mwinyi hatumii madawa ya kulevya ya aina yeyote.

“Mimi ni baba mzazi na wakala wa Mwinyi, huyu kijana hatumii aina yoyote ya madawa ya kulevya, nataka watanzania wajuwe kuwa kijana huyu hatumii tofauti na mitandao ya kijamii inavyosambaza taarifa za uzushi, mimi nipo tayari kwa mtu yeyote twende pamoja hospitali na kijana huyu tukampime kwasababu kama mtu anatumia madawa haya ataonekana tu hata kama kaacha kwa muda mrefu,” alifunguka baba mzazi wa Mwinyi.

Risiti ya malipo yaliyofanywa ili kumpima Mwinyi Haji damu na mkojo
Risiti ya malipo yaliyofanywa ili kumpima Mwinyi Haji damu na mkojo

Kwa upande wake Mwinyi amesema anaendelea vizuri tangu alipoumia katika mchezo dhidi ya MO Bejaia ya Algeria ambapo kwasasa yupo fiti na anafanya mazoezi na wenzake.

“Nashkuru Mungu naendelea vizuri tangu nilipoumia kule Algeria na tayari nishaanza kufanya mazoezi na wenzangu na nipo fiti”.

Wakati huohuo Mwinyi amethibitisha kuwa kweli walikwenda kupima kwa mkemia mkuu yeye na baba yake na ameonekana yupo salama.

“Ni kweli nilikwenda kwa Mkemia mkuu kupima mimi na baba na nimeonekanwa nipo salama, babaangu alikuja kunichukua wakati aliposikia taarifa kuwa natumia madawa, maana nililia sana na nilitaka hata kutoroka kambini kwasababu akili yangu ilikuwa haipo sawa kutokana na taarifa zilizozagaa kuwa mimi natumia madawa, niliumia sana na sijui nani nimemkosea hata ananifanyia hivi ila mimi nimeshamsamehe ndio changamoto za maisha lakini wameitia unyonge sana familia yangu, mama yangu alilia sana pamoja na dada zangu kuona nazushiwa taarifa hizi,” alisema Mwinyi huku akiwa anatokwa machozi.

Aidha Mwinyi amekanusha picha zilizozagaa sasaivi katika mitandao ya kijamii picha ambazo zimewekwa mbili kwa pamoja, moja ikionesha alivyokuwa zamani na moja alivyo sasa ambapo picha hizo zime tengenezwa si za kweli na yeye Mwili wake upo vilevile.

“Jamani mimi sipo hivyo kama picha zilivyozagaa katika mitandao ya kijamii, Kisandu ile picha ukiangalia tu unaona kama si ya ukweli, kwanza uwanja gani ule tulocheza mazoezi sisi Yanga, na ukiangalia kwa nyuma kuna goli la Hand ball, sasa sisi Yanga lini tumefanya mazoezi uwanja kama huo na pia Yanga wafanye mazoezi kusiwe hata mashabiki kuangalia!, duh watu wananichafua sana ila mimi nipo vizuri na wapenzi wa Yanga na Tanzania wategemee makubwa kuliko mwanzo Kisandu”.

Jumamosi ya April 30, 2016 moja ya Gazeti la michezo nchini Tanzania ambalo ni BINGWA liliandika taarifa ndefu kuhusu mlinzi wa Yanga ambapo kichwa cha habari kilikuwa kimeandikwa “SIRI NZITO YAFICHUKA YANGA”, NYOTA ALIYEMKUNA MAHREZ WA LEICESTER NI TEJA WA KUTUPWA, APIGWA CHINI”.

Zaidi ushahidi huo apo kwenye picha unaonesha kuwa Mwinyi hatumii madawa ya kulevya bali ni wachache wasiompenda wanamchafua.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>