Florentino Perez na Zinedine Zidane bado hawana muafaka juu ya nani aondoke kwenye kikosi ili kutoa nafasi ya Marco Asensio, kipenzi kipya cha Rais wa Real Madrid. Baada ya vita kubwa, Isco ndio imeamuliwa ampishe Asensio, kama alivyotaka Rais Florentino Perez.
Kwa mujibu wa AS, Madrid wamemuweka Isco sokoni. Mhispaniola huyo amechaguliwa kwa sababu za kibiashara zaidi. Zidane alitaka kumuacha Isco kikosini na kumuuza James Rodriguez, kwa sababu za kisoka.
Zidane amepoteza imani na James Rodriguez na anaamini Isco ana mchango mkubwa katika kikosi kuliko mcolombia huyo. PEREZ, kwa upande mwingine, ana macho kwa Mcolombia wake tu, anaamini James aliyemgharimu kiasi cha €80millons, bado ana thamani kubwa sokoni ikitokea akitaka kumuuza.
Madrid wapo tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya Isco, ingawa hawatomuuza kwa bei chee.