Na Baraka Mbolembole
MSHAMBULIZI wa Tanzania, Juma Ndanda Liuzio amekata tamaa ya kucheza michuano inayoendelea ya Caf Champions League 2016. Jina la Liuzio lilichelewa kutumwa kwa Shirikisho la soka Afrika-CAF.
Liuzio alikuwa majeruhi wa nyama za paja tangu Desemba 2015 na hakucheza hatua ya awali ya michuano hiyo mwaka huu kutokana na majeraha hayo lakini mara baada ya timu yake kufuzu kwa hatua ya makundi jina lake lilipelekwa CAF, Juni mwaka huu lakini inasemekana usajili huo ulichelewa kutumwa ndiyo maana hadi sasa Caf haijampa ruhusa ya kucheza michezo hiyo.
Zesco United wanahitaji ushindi mmoja tu katika game zao mbili zilizosalia ili wafuzu kwa nusu fainali kwa mara ya kwanza.
“Bado sijapata ruhusa ya kucheza. Sijui kama nitacheza tena michuano hii msimu hu,” anasema Liuzio ambaye timu yake itakuwa ugenini kucheza na Al Ahly ya Misri wikendi hii.