Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Historia ya wachezaji ghali zaidi England haitoi matumaini mazuri kwa Pogba

$
0
0

Uhamisho wa Paul Pogba Juventus kwenda Manchester United umevunja rekodi zote za ada za uhamisho wa wachezaji kwenye soka.  Lakini kilichotokea huko nyuma wakati vilabu vya Uingereza vinapovunja rekodi za usajili hakitoi matumaini sana.  
Hapa tuangalie wachezani sita ambao ada zao za uhamisho zilivunja rekodi lakini mwisho wao ndani ya vilabu vyao haukuwa mzuri. .

Angel Di Maria: Real Madrid – Man United, August 2014

Alisajiliwa kwa ada ya uhamisho wa £59.7 million
Mafanikio? Hakushinda taji lolote
Alikaa kwa muda gani? Msimu mmoja
Alifeli au alifaulu? Alifeli

Di Maria alikuwa mchezaji bora wa mchezo wa fainali ya UEFA Champions League kati ya Real Madrid na wapinzani wao Atletico na wakafanikiwa kushinda 4-1, baada hapo akasainiwa na United.  Magoli matatu katika mechi 5 za ligi ulikuwa mwanzo mzuri mno kwake ndani ya kikosi cha United, Lakini muargentina huyo hakuweza kufunga goli lingine katika michezo iliyofuata 22 ya ligi na hakuweza kufikia kiwango chake cha Real Madrid.  Di Maria alijiunga na  Paris Saint-Germain kwa ada ya uhamisho wa £44.3m msimu uliofuatia,  hasara ya  £15.4m for United.

 

Fernando Torres: Liverpool –  Chelsea, January 2011

Ada: £50m
Mafanikio? Champions League, Europa League, FA Cup
Alikaa kwa miaka mingapi: 4

Alifeli au Alifauli? Alifeli

Mshindi wa kombe la dunia na kombe la ulaya alikuwa na rekodi nzuri kwenye EPL akiwa na Liverpool katika kipindi cha miaka 3. Mafanikio yake ndani ya Liverpool yaliwashawishi Chelsea kutumia paundi millioni 50 kumsajili mhispaniola huyo.  Lakini mhispania huyo alifunga magoli 20 katika mechi 110 za ligi na baadae akaenda AC Milan kwa mkopo kabla ya kuhama kiujumla 2015..

 

Robinho: Real Madrid – Man City, September 2008

Ada ya uhamisho? £32.5m

Mafanikio: Hakushinda kikombe chochote 

Alikaa kwa muda gani? Miaka 2

Alifeli au alifaulu? Alifeli

Akiwa Real Madrid,  Robinho, alikuwa na nafasi ya kudumu katika kikosi cha timu ya taifa ya Brazil,  alisajiliwa katika kuonyesha dhamira ya kweli ya wamiliki wapya wa Manchester City katika kuijenga upya klabu hiyo. Baada ya kuanza vizuri,  akapoteza fomu yake na baada ya hapo akapoteza nafasi katika kikosi cha kwanza.  Akapelekwa kwa mkopo kwenye klabu yake ya zamani ya Santos kwa miezi y kabla ya kuuzwa kwenda AC Milan.

 

Andriy Shevchenko: AC Milan – Chelsea, May 2006

Ada? £30.8m1

Alishinda nini? FA Cup, League Cup

Alikaa kwa muda gani? Miaka 3

Alifeli au alifaulu? Alifeli

Nahodha wa Ukraine na mshindi wa Ballon D’OR alikuwa star wakati akiwasili Chelsea,  jambo lilomkosha Roman Abramovich lakini hali ilikuwa tofauti kwa kocha Jose Mourinho, ambaye hakumuamini katika mipango yake. Shevchenko alifunga magoli 9 katika mechi 47 za ligi na mwishowe akaishia kwenye benchi kabla ya kwenda Milan kwa mkopo na kisha kuhamia mazima Dynamo Kiev.

 

Rio Ferdinand: Leeds United –  Man United, July 2002

Alisajiliwa kwa kiasi gani? £30m
Alishinda? Champions League, 6 Premier Leagues, 3 League Cups
Alikaa miaka mingapi? 12
Alifaulu au alifeli? Alifaulu

Kijana wa miaka 23 wa Leeds United aling’ara akiwa na kikosi cha England na baadae akasainiwa na United na kuweka rekodi ya kuwa beki ghali zaidi duniani kwa mara ya pili. Kilichofuatia ni miaka 12 ya mafanikio na United na timu yake ya taifa kabla ya kuhamia QPR mnamo mwaka 2014.

 

Juan Sebastian Veron: Lazio –  Man United, July 2001

Alisajiliwa kwa kiasi gani? £28.1m
Alishinda nini? Premier League
Alikaa kwa muda gani? Miaka 2
Alifaulu au Alifeli? Alifeli

Sir Alex Ferguson alimuelezea Veron kama mmoja wa wachezaji bora duniani wakati alipomsajili. Mwishoni mwa msimu wake wa kwanza wa Muargentina huyo.  Ilifikia kipindi Fergie ilikuwa inambidi kupambana na waandishi wa habari ambao walikuwa wana mashaka na uchezaji wa Verone. Hata hivyo uhusiano wa kocha na mchezaji wake ulikuja kuharibika na ikabidi auzwe kwenda Chelsea kwa £15m.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles