Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

BAADHI YA VILABU VYAANZA KUMFUKUZIA MATA

$
0
0

Juan Mata

Inaripotiwa kwamba, klabu ya Fenerbahce imeonesha nia ya kutaka kumsaini kiungo wa Manchester United Juan Mata.

Mhispania huyo amejikuta kwenye sitofahamu ndani ya Old Trafford kufuatia kutua kwa Jose Mourinho kama manager na inasemekana tayari ameshapokea ombi la Fenerbahce kumtaka Mata.

Mata alionekana kuchukizwa na kitendo cha Mourinho kuammua kumpumzisha dakika 30 baada ya kuingia uwanjani kwenye mchezo wa Jumapili wa Ngao ya Jamii dhidi ya Leicester kisha baadae Mourinho akaeleza aliamua kufanya hivyo kutokana na na kimo cha Mata.

Everton imehusishwa pia na dili hilo la kumtaka kiungo huyo mwenye miaka 28 lakini gazeti la Uturuki (Milliyet) linadai kuwa, Fenerbahce pia wanania ya kumsajili nyota huyo wa zamani wa Chelsea kwa ada ya uhamisho wa £20m ili kuziba nafasi ya Nani ambaye amejiunga na Valencia.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>