Kiungo mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs Dele Alli, amebadilisha jina litakalotumika kwenye jezi yake mgongoni msimu huu kwasababu haoni uhusiano wa moja kwa moja na jina la Alli na sasa atakuwa akitumia jina na Dele kuanzia msimu huu.
Awali Dele Alli alikuwa akitumia jina la Alli mgongoni mwa jezi yake msimu uliopita vilevile kwenye michuano ya Euro 2016.
Alli, 20, amesema: “Nataka niweke jina kwenye jezi yangu ambalo lina uhusuiano wa moja kwa moja na mimi, jina ambalo linaniwakilisha mimi kama nilivyo na nahisi jina la Alli halina uhusiano wa moja kwa moja na mimi.
“Huu sio uamuzi ambao nimekurupuka tu kufanya bali ni uamuzi ambao umeridhiwa na familia nzima kwa ujumla.”
Sababu kubwa za maamuzi hayo inaelezwa kwamba, baba yake Dele Ali ambaye alikuwa akiitwa Kenny Alli mwenye asili ya Kinigeria, hakuhusika katika malezi ya mwanaye na hivyo kupata shida katika makuzi yake kutokana na mama yake kuwa mlevi kupindukia.