Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Jicho la 3: ILISHAWAKUTA, SAMATTA, TAMBWE, HANS, NGAO YA AZAM FC NA MEDALI ZAO NI ISHARA YA MSIMU MWINGINE MBOVU

$
0
0

Ngao

Na Baraka Mbolembole

NANI anayehusika na uandaaji wa tuzo, vikombe na medali za washindi katika ligi/mashindano ya hadhi ya juu Tanzania Bara? Anasubiri nini kujiuzulu? Ama kweli, ‘Tanzania Football Fitna a.k.a ‘Tifuatifua’ imekosa watu makini, haina watu wa mpira.

Amis Tambwe alipewa ‘kiatu feki cha dhahabu’ ambacho ni zawadi yake binafsi baada ya kuibuka mfungaji bora wa ligi kuu Tanzania Bara msimu uliopita!

Hata mwezi sidhani kama umepita tangu raia huyo wa Burundi kukabidhiwa kiatu kilichokuwa ‘kimepakwa rangi za nyumba.’ Juzi Jumatano mabingwa wapya wa Ngao ya Jamii, timu ya Azam FC ‘walifedheheshwa’ sana na zawadi yao hiyo ya ‘kioo kilichowekwa karatasi juu yake.

Baada ya mechi nzuri iliyoambatana na kujituma kwa nguvu, akili na maarifa binafsi ya wachezaji na mabenchi ya ufundi, dakika 90′ zikazalisha magoli manne maridadi kuashiria washambuliaji wanarudi na moto, Shomari Kapombe anarejea na mwili mkubwa, uwezo uleule na usongo wa kufunga magoli akitokea katika beki.

Ngao 1

Lakini ukiachana na magoli ‘chap-chap’ ya Mzimbabwe, Donald Ngoma-moja la mkwaju wa penalti aliyoitafuta mwenyewe dakika ya 22′ na lile la uwezo binafsi dakika moja baadae, kisha urejeo wa ki-mipango wa Azam FC, goli la mpira wa kona la Kapombe dakika 15 kabla ya kumalizika kwa mechi.

Na lile la mkwaju wa penalti lililofungwa dakika ya mwisho ya mchezo na nahodha wa timu hiyo, John Bocco ni wazi mambo mengi ya kiutendaji yataendelea kuathiri ligi.

TFF ndipo yanapozaliwa na kuundwa matatizo mengi yanayopelekea kushusha hadhi ya kiushindani, na hadhi ya ligi yenyewe. Unawezaje kutoa Ngao feki siku chache baada ya vyombo vya habari na wadau wa mchezo wenyewe kupiga kelele za kiatu cha mtumba kiliitwa chadhahabu?

Ni maswali yanayoacha majibu ya kusikitisha tu. Nasikia kuna kituo kimoja cha TV ambacho kimeshinda tenda ya uoneshaji wa VPL msimu unaoanza Jumamosi hii kilishindwa dau na kituo kingine licha ya awali kushinda.

Yaani, walitokea walioonyesha game hiyo siku ya Jumatano na kuweka dau la kufuru ambalo lilivuruga ofa ya vinara wa urushaji matangazo ya TV katika ligi ya VPL.

IMG_0323

Inamaanisha kuwa TFF iko makini sana katika mipango ya ukusanyaji wa mapato kupitia game za timu za VPL lakini inakuwaje wanakuwa na maandalizi hafifu katika zawadi za washindi?

Ni kwanini medali za washindi wa Ngao ya Jamii 2016 timu ya Azam FC zilikuwa ni za mabati yaliyopakwa rangi ya dhahabu na si angalau madini ya shaba? Kama hawatoi medali zenye madini halisi ni vyema wakatangaza kwa umma ili ijulikane!

Medali 2016 feki, Ngao ya Jamii 2016 feki, kiatu cha dhahabu 2015/16 kikawa cha mtumba! Weee! Jamaa na timu yako inayoandaa zawadi za washindi naomba ujiuzulu tafadhali, imetosha sasa.

Jina la Samatta lilishawahi kuambatana na picha ya Mzambia, Rainfrod Kalaba, hata ‘Hans van der Pluijm’ mlichemka. Naona itafika hatua sasa mtakosea hadi jina linalowawakilisha-TFF.

Jicho Langu la 3 Ilishawakuta, Samatta, Tambwe, Hans, Ngao ya Azam FC na medali zao ni ishara ya msimu mwingine utakaoharibiwa na watendaji wa TFF.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>