Ligi kuu ya soka Tanzania bara imeendelea leo kwa mchezo mmoja kati ya Kagera Sugar waliokuwa wenyeji wa Mbeya City katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga mchezo uliomalizika kwa sare ya bila kufungana.
Mechi hiyo ilikuwa ni ya sita kupigwa baada ya mechi tano kuchezwa siku ya ufunguzi wa ligi Jumamosi Agosti 20. Hadi sasa timu 12 zimeshajitupa uwanjani huku timu nne pekee zikiwa bado hazijacheza michezo yao kutokana na sababu mbalimbali.
Jumatano Agosti 24 Mbao itacheza dhidi ya Mwadui FC kwenye uwanja wa CCM Kirumba wakati mabingwa watetezi wa ligi hiyo Yanga SC wao watakipiga pindi watakaporejea kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya mchezo wa kimataifa dhidi ya TP Mazembe.
Simba wanaongoza msimamo wa VPL kwa tofauti ya magoli mbele ya Ruvu Shooting na Tanzania Prisons ambazo zilipata pointi tatu kwenye mechi zao za kwanza za ligi.
Msimamo kamili wa VPL ni kama unavyoonekana kwenye chati hapa chini