Beki wa kulia wa Ndanda FC Aziz Sibo amefungwa Plaster of Paris (P.O.P) baada ya kuumia kifundo cha mguu wake wa kushoto wakati wa mchezo dhidi ya Simba Jumamosi iliyopita kwenye uwanja wa taifa.
Sibo alilshindwa kuendelea na mchezo na kulazimika kutolewa na machela baada ya kupata maumivu dakika ya 65 na nafasi yake ikachukuliwa na Bakari Mtama. Katika mchezo huo, Ndanda ilijikuta ikipoteza mchezo wake wa kwanza wa ligi kwa kipigo cha magoli 3-1 kutoka kwa Simba.
Jeraha hilo litamweka Sibo nje ya uwanja kwa muda wa mwezi mmoja huku akikosa mechi kadhaa za ligi kuu zitakazoihusisha timu yake.