Mfungaji wa muda wotekwenye klabu ya Chelsea Frank Lampard ambaye kwasasa anaitumikia New York City FC ya Marekani amesema siku moja atarejea kwenye Stamford Bridge.
Lampard ali-comment hivyo wakati akifanyiwa interview na mtandao rasmi wa New York City FC.
Kiungo huyo alijibu swali aliloulizwa na shabiki kwenye account yake ya mtandao wa twitter, ambapo shabiki huyo alimuuliza Lampard kama anampango wa kurudi Chelsea baada ya kustaafu soka.
Kwakifupi, Lampard alielezea namna anavyopenda siku moja kurejea Stamford Bridge.
Siku moja nitarejea Chelsea. Sina uhakika kama nitakuwa na nafasi ya kufanya kazi, hilo ni jukumu la klabu. Nitafurahi kama nitapewa jukumu la kufanya.
Haijalishi kama nitapewa jukumu au la, nitahudhuria mara kwa mara kuangalia mechi za Chelsea kwasababu ninaipenda klabu na kunakitu kinaniunganisha moja kwa moja.