Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

ANAWEZA KUWA HAZARD MPYA? SOUTHAMPTON YAMTWAA SOUFIANE BOUFAL

$
0
0

boufal

Inawezekana kabisa kukawa na wachezaji wengi vijana am ao wamekuwa wakifaanishwa na wachezaji wengi wakubwa lakini mara nyingi ikiwa ni wachezaji wawili wanaotikisa dunia yaani Cristiano Ronaldo au Lionel Messi.

Wachezaji wengi wamekuwa wakifananishwa na hawa kwa sababu ya wao kuwepo kwa muda mrefu kwenye kiwango bora hali inayowafanya kuwa role models wa wachezaji wengine.

Lakini umelisikia jina jipya ndani ya Southampton? Ndio, Southampton wametangaza kumsajili mchezaji Soufiane Boufal wakimtwaa kwa rekodi ya usajili ndani ya klabu hiyo, paundi milioni 16.

Boufal ni winga na kama wewe ni shabiki wa Eden Hazard basi namzungumzia mchezaji ambaye wamefanana sana kiuchezaji na hata vilabu walivyotoka. Boufal, 22, anatoka klabu ya Lille ambayo ndiyo Hazard alikowika kabla ya kutua darajani pale Stamford Bridge.

Boufal ni mchezaji anayependa sana kukimbia na mpira mguuni, anajua kufunga kwa kiasi lakini pia akiwa si mchoyo kwa maana ya kutoa pasi za mwisho. Ni mzuri wa mipira ya kufa na ana kasi nzuri jambo linalomfanya kuwa mwepesi kuingia kwenye eneo la 18.

Jukumu kubwa kwake litakuwa kukubaliana na ugumu wa ligi hii na aweze kuendana na kasi yake maana kuwa Eden Hazard sio jambo dogo, huku pia ligi kuu ya Ufaransa, Ligue 1 ikiwa haishabihiani na Ligi kuu ya nchini Uingereza.

Je atakuwa Hazard mpya? Mimi naamini anaweza kuja kuwa mchezaji muhimu sana na naviona vilabu vingi vikimgombania kwa kiasi mara mbili ya alichonunuliwa nacho.

Mtizame hapa.

Niffolow Instagram @nicasiusagwanda


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>