Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

BARCELONA WAMEKAMILISHA USAJILI WA MCHEZAJI MWINGINE

$
0
0

VALENCIA, SPAIN - JANUARY 03:  Paco Alcacer of Valencia celebrates scoring his team's second goal during the La Liga match between Valencia CF and Real Madrid CF at Estadi de Mestalla on January 03, 2016 in Valencia, Spain.  (Photo by Manuel Queimadelos Alonso/Getty Images)

Barcelona imethibitisha kumsaini Paco Alcecar kutoka Valencia kwa mkataba wa miaka mitano, nyota huyo kwenye miaka 23 amehamia Nou Camp kwa ada ya uhamisho wa euro milioni 30 huku kukiwa na kipengele cha Barcelona kuongeza euro milioni mbili za ziada.

Alcacer amekuwa mchezaji wa nne kwa miaka ya hivi kiaribuni kutoka Valencia na kujiunga na Barcelona akiungana na mlinzi Jordi Alba (2012) na Jeremy Mathieu (2014) pamoja na Andre Gomes ambaye amejiunga na Barca kwenye majira haya ya usajili.

Amefunga magoli 13 na kutoa assists sita akiichezea Valencia msimu uliopita huku akiwa mfungaji bora wa timu ya taifa ya Hispania katika mbio za kwania kufuzu kucheza fainali za Euro 2016 baada ya kufunga magoli matano.

Alitemwa kwenye kikosi cha mwisho kilichosafiri kwenda Ufaransa kwenye mashindano ya Euro 2016.

Alcacer hakujumuishwa kwenye kikosi cha Valencia kilichocheza dhidi ya Eibar Jumamosi iliyopita. Baada ya kichapo cha goli 1-0, kocha wa Valencia Pako Ayesteran aliwambia waandishi wa habari mchezaji huyo hakuwa kwenye wakati mzuri wa kushindana.

Usajili wa Alcacer umeangukia siku ambayo anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa (August 30) ambapo ametimiza miaka 23.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>