Na Athumani Adam
Miongoni mwa habari kwenye soka hapa nchi ni suala la Azam kucheza mechi dhidi ya timu kongwe Simba na Yanga kwenyye uwanja wa Azam Complex kule Chamanzi. Wakati sakata la Azam likiendelea kupamba moto, kumbe hata Ulaya zipo timu ambazo zinacheza mechi zake kwenye viwanja ambavyo vinabeba mashabiki sawa na ule uwanja wa Chamanzi au kuzidi kidogo.
Makala hii inakupa timu sita ambazo zinacheza mechi zake kwenye viwanja vidogo kutoka kwenye ligi nne kubwa duniani.
- EIBAR (Spanish La liga) Ipurua Municipal, watu 5250
Ni uwanja unaomilikwa na Mamlaka ya jiji la Eibar. Ulijengwa mwaka 1947 pia unatumiwa kwenye michezo mbali mbali hususani mpira wa miguu.
- LEGANES (Spanish La Liga), Municipal De Butarque, watu 8000
Uwanja huu unapatika katika jiji la Madrid eneo la Leganes, ulijengwa kati ya mwaka 1997-1998. Klabu ya CD LEGANES inatumia uwanja huu kucheza mechi zake za nyumbani.
- CROTONE (Serie A), Ezio Scida, watu 9631
Kwenye mji mdogo wa Crotone kule Italy, kuna uwanja ambao unatumiwa na timu ya Crotone ujilikanao kwa jina la Ezi scida. Uwanja huu umepewa jina hilo kwa heshima ya mchezaji wa zamani aliyejulikana kwa jina Ezi Scida.
- AFC BOURNEMOUTH (English Premier league), Vitality, watu 12000
Kutokana na masuala ya udhamini sasa unajulikana kwa jina la Vitality badala ya Dean Court. Ulijengwa mwaka 1910 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2001
- INGOLSTADT (Bundesliga), Audi- Sportpark, watu 15000
Ni uwanja uliojengwa mwaka 2010 kwa thamani ya euro milioni 20. Klabu ya Ingolstadt 04 inatumia uwanja huu kucheza mechi za nyumbani
- CAGLIARI (Serie A), Sant’elia-, watu 16000
Ulifunguliwa rasmi mwaka 1970, unatumiwa na klabu ya Cagliari calico. Uwanja huu upo chini ya mamlaka ya mji wa Cagliari.