Timu ya taifa ya El Salvador imedai kwamba wamekataa rushwa ya fedha waliyoahidiwa ili wapoteze mchezo wa leo jumanne wa kugombea kufuzu kucheza kombe la dunia 2018 vs Canada.
Katika mkutano wa waandishi wa habari, wachezaji wa timu hiyo waliicheza sauti waliyoirekodi ya mtu aliyekuwa akiwahidi mlungula ili wapange matokeo.
Canada inawalazimu kuwafunga El Salvador – ambao hawawezi kufuzu, na kuombea Mexico wawafinge Honduras katika mchezo wa mwisho wa kundi A ili wao waweze kusonga mbele.
Shirikisho la soka duniani Fifa limethibitisha kwamba limeanza uchunguzi juu ya suala hilo.
Mwandishi wa habari mchunguzi, Declan Hill amezungumza na kusema mwamba ofa hiyo ya mlungula ilitolewa na mtu kutoka El Salvador ambaye anafahamiana na baadhi ya wachezaji, lakini ilikuwa ni kwa madhumubi ya kuisadia timu ya taifa ya Honduras.
Shirika la habari ya Uingereza BBC lilimtafuta msemaji wa Shirikisho la soka la Honduras kujibu tuhuma hizi bila mafanikio.
Msemaji wa FIFA kwa upande amesema kwamba wanafahamu juu tukio hilo na sasa wanashirikiana na vyombo vya dola husika kuchunguza tuhuma hizo.
Canada, El Salvador, Honduras na Mexico ni wanachama wa shirikisho la Amerika ya Kaskazini, kati na Visiwa vya Caribbean (Concacaf).
Mataifa matatu yaliyo chini ya Concacaf yatafuzu moja kwa moja kushiriki mashindano ta 2018 World Cup, yatakayofanyika nchini Russia na timu ya 4 itafuzu kupitia mtoano na timu kutoka ASIA.