Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Video: Mshambuliaji wa Everton azuga kaumia uwanjani kukwepa kukamatwa na polisi

$
0
0

enner-valencia

Ecuador iliwafunga Chile ambao ni mabingwa mara mbili wa kombe la bara la Amerika Kusini katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia siku ya Alhamisi lakini matokeo hayo yalifunikwa na mambo kadhaa yaliyojiri mwishoni mwa mchezo huo.

Magoli ya Antonio Valencia, Cristian Ramirez na Felipe Caicedo yaliipa Ecuador ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Chile kikosi ambacho kimeshinda mara mbili mfululizo taji la Copa Amerika.

Mshambuliaji wa Everton Enner Valencia anayekipiga West Ham kwa mkopo, alianza kwenye mchezo huo na alitoa assist kwa Antonio Valencia aliyefunga goli la kwanza katika mechi hiyo.

Naweza kusema kwamba, Enner Valencia alikuwa na mambo mengi kichwani mwake wakati mchezo huo wa kutafuta kufuzu fainali za Kombe la Dunia ukiendelea.

Imethibitika kwamba, wiki hii polisi nchini Equador walijaribu kumkamata Valencia kutokana na kutolipa kiasi cha dola la 17,000 za Marekani ambazo ni gharama za matunzo ya binti yake mwenye miaka mitano.

Lakini mshambuliaji huyo hakwenda kituo cha polisi baada ya maofisa wa polisi kushindwa kufuata taratibu na kumpa Valencia mwanya wa kuepuka sekeseke hilo.

Zikiwa zimesalia dakika 10 mchezo kumalizika, wakati huo polisi wakiwa nje ya pitch wakisubiri kumkamata Valencia baada ya mchezo, mshambuliaji huyo wa Everton alijiangusha na kujifanya amepata majeraha.

Valencia akabebwa kwenye stretcher, lakini picha zinaonesha kuwa polisi wakamfatilia mshambuliaji huyo wa Ecuador ili wamkamate.

Ianadaiwa kuwa, viongozi wa kikosi cha Ecuador walijaribu kuwazuia polisi kuhakikisha Valencia anarudi kwanza kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kabla ya kukamatwa na polisi.

Benchi la ufundi nalo likatoa sharti kwamba, polisi wanatakiwa kuhakikisha mchezaji wao atarejea kwenye hoteli waliofikia wachezaji wa timu ya taifa ya Ecuador.

Saa chache baadaye, mwanasheria wa Valencia alifanikiwa kumshawishi Jaji kusitisha amri ya kukamatwa kwa mchezaji huyo.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>