Magoli ya Mzamiru Yassin na Shiza Kichuya yameendelea kuiweka Simba kileleni mwa ligi kuu Tanzania bara ikifikisha jumla ya pointi 23 baada ya kucheza mechi 9 hadi sasa.
Mzamiru Yassin alianza kuifungia Simba goli la kwanza dakika ya 43 kipindi cha kwanda akiunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Shiza Kichuya.
Simba ikafanikiwa kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0 dhidi ya wapinzani wake Kagera Sugar.
Kichuiya akapachika bao la pili dakika 75 kwa mkwaju wa penati baada ya Ibrahim Mohamed kuangushwa kwenye eneo la hatari la Kagera Sugar.
Dondoo
- Simba bado inaendeleza rekodi yake ya kutopoteza mchezo wa VPL msimu katika mechi 9 ilizocheza. Imetoka sare mara mbili na kushinda michezo mingine 7.
- Kichuya amefikisha magoli 7 katika mechi 9 za VPL mabazo ameitumikia Simba tangu alivyojiunga nayo akitokea Mtibwa SUgar ya Morogoro.
- Maoli yote ya Simba dhidi ya Kagera Sugar yamefungwa na wacheaji wa zamani wa Mtibwa Sugar (Mzamiru Yassin na Shiza Kichuya).
- Simba imeshinda mechi 4 kati ya mechi 5 za mwisho ambazo wamekutana na Kagera Sugar, Kagera Sugar wameshinda mechi moja dhidi ya Simba katika mechi 5 zilizopita. (Simba 0-1 Kagera Sugar, Kagera Sugar 1-2 Simba, Simba 3-1 Kagera Sugar, Kagera Sugar 0-1 na Simba 2-0 Kagera Sugar)