Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Mambo matano ya kujifunza baada ya michezo ya EPL October 15

$
0
0

silva-vs-everton

1. Manchester City inacheza pale Kevin De Bryune anapokuwa kwenye kiwango bora. Ni mapema sasa Guardiola anatakiwa kutafuta namna ya kurejesha muunganiko wa Silva na Aguero.

2. Walcott ataendelea kunufaika sana na uwepo wa Sanchez kama mshambuliaji wa mwisho. Sanchez anafanya timu katika eneo la mwisho kuwe na free flowing football (mtiririko huru wa mpira) hivyo kutokutulia kwake katika nafasi moja kunamfanya Walcott awe kwenye nafasi muda mwingi.

3. Kama ulikuwa hujahesabu jina la Tottenham kwenye orodha yako ya ubingwa basi waweke. Ndio timu iliyokamilika zaidi kwa maana ya uwiano wa eneo la ulinzi mpaka eneo la ushambuliaji.

4. Unaweza kujiuliza kwanini Leicester City wanafanya vyema ligi ya mabingwa Ulaya na sio ligi kuu ya England. Advantage waliyopata msimu uliopita ndiyo wanayoitumia kwenye UEFA msimu huu. Hawajulikani vyema falsafa zao za counter attacks kule. Muunganiko aliowapa Kante utaendelea kuwahukumu lakini pia Vardy na Mahrez wamesahau viatu vyao kwenye gari walizokuwa wanatumia msimu uliopita kabla ya kupata BMW za tajiri.

5. Kuna kitu Victor Moses anaweza kumpa Conte msimu huu. Anaonekana kuwa tofauti, ana njaa na anayeweza kukupa matokeo tofauti na Willian ambaye ametumika mfulululizo sana na kwa kipindi kirefu. Costa hatoacha kufunga kipindi hiki cha Conte lakini ili Chelsea wawe wanaogombania ubingwa inabidi Hazard arejee na Oscar atuzibie lile pengo la Fabregas. Pasi za Fabregas bado hazionekani uwanjani. Ingawa bado najiuliza Luiz, Luiz, Luiz. Acha niendelee kukupa muda.

Nicasius Nicholaus Agwanda (Coutinho Suso).

Soma Mwananchi kila Jumatatu na Jumapili. Kuna makala zangu bora, ukurasa unaitwa Gozi la ng’ombe.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles