Licha ya kufungwa na Bayerm Munich lakini bado Borussia ipo vizuri kwenye msimamo wa ligi ambapo inashika nafasi ya pili kwenye mbio za ubingwa wa Bundesliga. Sasa kesho saa tatu na nusu usiku kupitia StarTimes itaonekana Live Match kati ya hizi timu mbili ambapo kocha wa sasa wa BVB Thomas Tuchel anaijua vizuri timu anayocheza nayo vizuri Mainz.
Kabla ya kuanza kuifundisha BVB, Thomas Tuchel alikua ndie kocha mkuu wa Mainz O5 na baada ya Klopp kuacha kufundisha Borussia akapewa mikoba.
Sasa kesho ndio anakutana na timu hiyo ya zamani akiwa na lengo moja tu la kuichapa.Kocha huyu anasifika sana kwa kuwa na mbinu anategemea kupata ukaribisho mzuri tu kutoka kwa mashabiki wa Mainz 05 kwenye uwanja wao wa nyumbani lakini bado anaitaji kuwafunga.
Watu wengi wanaipa nafasi Borussia kushinda mechi hii kutokana na kuwa na timu nzuri na kocha Thomas Tuchel anaijua vizuri timu pinzani ambayo ni Mainz 05.
Kivutio kwenye mechi hii zaidi ya kocha huyu ni mchezaji Aubameyang ambae tangu msimu uanze amekua akitupia kwenye kila mechi anayocheza. Swali ni kwamba ataendeleza hiyo rekodi yake hadi lini?. Mechi ya Bayern ilikua ya mwisho au ataendeleza kwenye hii mechi. Basi hakikisha king’amuzi cheko cha StarTimes kimelipiwa na unacheki burudani hii ukiwa umetulia nyumbani na familia.