Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Uongozi umemuomba Hans van Pluijm kuendelea kuifundisha Yanga

$
0
0

img-20161028-wa0003

Zikiwa zimepita siku nne tangu kocha mkuu wa Yanga Hans van Pluijm kuamua kuandika barua ya kujiuzulu kuifundisha klabu ya Yanga, uongozi wa klabu hiyo leo October 28 umemuandikia barua kumuomba Hans abadili maamuzi yake na kurejea kwenye benchi la ufundi kuendelea na majuku yake kama kawaida.

Kwa mujibu wa habari za ndani ya Yanga, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba alikutana na Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Baraka Deusdedit pamoja na Hans van der Pluijm na kumshawishi kocha huyo raia wa Uholanzi kuachana na uamuzi aliouchukua awali.

Mh. Nchemba ambaye ni shabiki mkubwa wa Yanga amekuwa karibu na klabu hiyo tangu Hans alipotangaza kujiuzulu nafasi yake. Siku moja kabla ya mchezo kati ya Yanga na JKT Ruvu, Mh. Nchemba aliwatembelea wachezaji kambini na kuzungumza nao ikiwa ni pamoja na kuwatia moyo kutokana na kuondokewa na kocha wao.

Yanga imecheza mchezo mmoja bila ya Hans ambaye siku hiyo alikuwa jukwaani akiishuhudia ikipata ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya JKT Ruvu kwenye uwanja wa Uhuru.

Hans aliandika barua ya kujiuzulu nafasi yake baada ya ujio wa kocha wa Zesco United George Lwandamina huku ujio wake ukihusishwa kuja kuchukua majukumu ya Babu Hans aliyeipa Yanga ubingwa ligi kuu Tanzania bara mara mbili mfululizo, taji la FA na kufikisha klabu hiyo hatua ya robo fainali ya kombe la shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza tangu miaka 18 iliyopita.

img-20161028-wa0005


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>