Wengi wakisikia jina la mchezaji Dwayne Wade, akili na fikra zinakuwa kule suth beacg, Miami ambako ndiko alikojitengenezea jina mpaka kuitwa mr. Miami na kisha kuchukua ubingwa wa NBA mara tatu tofauti, mbili akiwa na mchezaji ambaye pia ni rafiki yake, Lebron James.
Lakini baada ya kutofautiana na Pat Riley, Rais na mkurugenzi mkuu wa masuala ya ufundi wa Miami Heat, Dwyane Wade aliamua kutimkia zake Chicago Bulls ambako ndiko nyumbani kwao ili pengine amalizie maisha yake ya mchezo wa NBA huko.
Na katika mchezo wake wa kwanza ndani ya jezi hizi maarufu alizowahi kuvaa mchezaji bora wa muda wote, Michael Jordan, Dwayne Wade wala hakuwaangusha watu. Wade alifanya kile ambacho wengi wanategemea kukipata kutoka kwake hasa wakati huu ambao Chicago Bulls imeaacha Rondo, Joakhim Noah na kuwaleta Wade na Rondo.
Wade alifunga jumla ya pointi 22 katika ushindi wake wa kwanza na katika mechi yake ya kwanza akiwa na Chicago, Jimmy Butler akaongeza pointi 24 na kuisaidia Chicago Bulls kuichapa Boston Celtics 105-99.
Isaiah Thomas aliiongoza klabu ya Boston akiwa na alama 25 huku mchezaji Avery Bradley akifunga alama 16, na pia Jae Crowder akifunga pointi 14 points lakini haikuwa rahisi kwa Celtics ambayo haikuwa vizuri baada ya ushindi dhidi ya BBrooklyn Nets.
HIGHLIGHTS