Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Mkude amefichua siri ya mafanikio Simba

$
0
0

img_4774

Kikosi cha Simba bado kipo mkoani Shinyanga kikiendelea kujiandaa na mchezo wake wa pili katika mkoa huu baada ya kucheza na Mwadui Jumamosi iliyopita, Jumatano November 2 Stand United watakuwa wenyeji wa Simba kwenye uwanja wa Kambarage.

Kabla ya mchezo huo kupigwa, www.shaffihdauda.co.tz  imefanya mahojiano na nahodha wa Simba Jonas Mkude ili kujua mambo mbalimbali ndani ya kikosi hicho ambacho kwa sasa kinafanya vyema kwenye ligi kuu Tanzania bara kikiwa kinaongoza ligi kwa alama 32 baada ya kucheza mechi 12 huku kikiwa hakijapoteza mchezo hata mmoja.

Mahojiano haya yamejikita kwenye timu kufanya vizuri na nafasi ya Mkude kama nahodha kuhamasisha wachezaji wanzake kuhakikisha wanaipa Simba ubingwa kwa mara ya kwanza baada ya kuukosa katika misimu ya hivi karibuni.

Ikumbukwe, Jonas Mkude na Mwinyi Kazimoto ndio wachezaji pekee wa Simba waliovaa medali za ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara Simba ilipotwaa taji hilo kwa mara ya mwisho.

Siri ya mafanikio ya Simba msimu huu (2016/17)

Mmepata ushindi mkubwa ugenini kwa miaka ya hivi karibuni, mnazifunga kwa magoli mengi timu ambazo awali ziliwapa changamoto. Mmlishinda dhidi ya Toto Africans timu ambayo ilikuwa ni ngumu kwa Simba, mkapata ushindi mwingine dhidi ya Mwadui timu ambayo msimu uliopita iliwapa changamoto. Nini siri ya haya yote?

Msimu huu tumejipanga vizuri kuanzia tulivyoanza maandalizi. Umoja uliopo kuanzia kwa mwalimu na wachezaji, viongozi na mashabiki ndio chachu ya haya yote yanayotokea.

Wachezaji wapya chachu ya mafanikio Simba

Wachezaji wapya walioongezwa kwenye timu unadhani ndiyo silaha kubwa kwa sasa kwasababu magoli 24 yaliyofungwa na Simba, 21 yamefungwa na wachezaji wapya, unadhani ujio wao umeengoza nguvu kwenye kikosi?

Siri ya wao kusajiliwa Simba lazima viongozi walikuwa wanahitaji vitu kutoka kwao, tumekaa muda mrefu bila kupata ubingwa. Wameziba mapengo  ambayo waliyaona msimu uliopita yaliyosababisha sisi tukashindwa kufanya vizuri. Kwahiyo usajili wao umeongeza ushindani kwenye kikosi na hiyo inafanya kuwa na kikosi kipana kwasababu mtu anaeanza hana tofauti na aliyepo kwenye benchi ila inakuwa ni mpango wa mwalimu kumuanzisha nani kutokana na kitu anachotaka kutoka kwenye mechi husika.

Partnership ya Mkude, Muzamiru na Kazimoto

Mara nyingi umecheza na Muzamiru Yassin kwenye eneo la katikati sambamba na Mwinyi Kazimoto ambaye anatokea pembeni lakini anaingia ndani, unadhani hii imetengeneza partnership nzuri?

Kwa falsafa ya mwalimu anaona mimi, Mzamiru na Mwinyi tunafaa kucheza pamoja wakati mwingine anaweza akaanza Mnyate au Ibrahim Mohamed. Kwahiyo mwalimu anajaribu kuchanganya watu tofauti kulingana na falsafa anayoitaka.

Kupatikana kwa ITC ya Musa Ndusha kunaweza kukaongeza kitu ndani ya timu?

Ni kitu kizuri kwasababu anakuja kuongeza ushindani Musa ni mchezaji mzuri kwahiyo anatakiwa awe tayari kiakili kwa ajili ya kushindana kupata nafasi. Akipambana anaweza kupata nafasi na kuisaidia timu.

Gape la pointi 5 linaiweka Simba kwenye nafasi gani katika mbio za ubingwa

Kuna gape la pointi 5 na timu inayowafata nyuma, unadhani mtaweza ku-maintain hilo gape hadi manamaliza raundi ya kwanza ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kushinda ubingwa?

Timu inaweza kuchukua ubingwa hata kwa tofauti ya pointi moja, pointi tano ni nyingi sana kwenye mpira. Wao wamejipanga na sisi tmejipanga pia, kila mechi tutazidi kupambana ili kufanya vizuri nadhani Mungu akitusaidia tunaweza tukarudia rekodi yetu ya kuchukua ubingwa bila kupoteza mechi.

Mitihani iliyopo mbele kabla ya Simba kutwaa ubingwa

Kwa uzoefu wako wa miaka minne kwenye ligi kuu Tanzania bara, unadhani kuna mitihani gani mbele yenu ambayo inabidi muishinde kabla ya kutwaa ubingwa?

Ligi ni ngumu, huwezi kuchagua timu kwasababu kila timu imejipanga ndiyomaana kila mechi kwetu tunapambana bila kujali tunacheza na timu gani. Timu zote zimejipanga kwahiyo hatuangalii Azam, Yanga wala Mtibwa kwasababu kupata matokeo ni shida. Timu kama Stand imeifunga Yanga, ikaifunga Azam ndiyo maana ligi inakuwa ngumu sana.

Ratiba imebana sana, kwahiyo kama hukujiandaa vizuri kabla ya ligi inakuwa shida kidogo kwasababu kila baada ya siku tatu tunacheza mechi. Inachosha lakini haina jinsi ratiba tayari imeshapangwa kwahiyo kila mechi tunapambana kupata matokeo.

Bonus nzuri kila timu inaposhinda

Tunasikia mnapata bonus nzuri kwa mechi ambazo mnashinda, ukiwa kama nahodha nafasi yako ni ipi kuhakikisha wachezaji wenzako wanajituma  zaidi?

Wote tumekutana hapa kwa ajili ya Simba, hakuna asiyejua majukumu yake, tumejuana na kufahamiana kwasababu ya Simba, wote tuliopo kwenye timu tunahitaji kupata nafasi lakini upambanaji wa mtu ndiyo unaweza kumpa nafasi kilichopo ni kukumbushana majukumu ili kuifikisha Simba inapotaka kuwa.

Mkataba wa Mkude upo ukingoni

Mwisho wa msimu huu mkataba wako utakuwa unamalizika, unadhani baada ya mechi hizi tatu zilizosalia kumalizika kwa raundi ya kwanza na ligi kusimama ndiyo itakuwa muda mwafaka kwako kumaliza maswala ya mkataba wako na Simba?

Siwezi uzungumzia hilo kwasababu bado nipo kwenye mkataba na Simba, ni jukumu la viongozi kuangalia kama bado wananihitaji kuendelea kuwepo Simba au wakiona sina msaada wataniachia niondoke lakini kwa sasa siwezi kuzungumzia makataba kawasababu nipo ndani ya mkataba.

Ungependa kuona mkataba wako mpya ukiwa na ofa ya ziada kwa kiasi gani ukilinganisha na iliyopita?

Siwezi kulisemea hilo kwasababu bado nipo kwenye mkataba halafu bado ligi inaendelea. Watakapoona mimi nahitajika kuendelea kuwepo, tutakaa chini na kuongea.

Kunyanyua ubingwa wa VPL 2016/17

Ukiwa kama nahodha, endapo Simba itafanikiwa kutwaa ubingwa ligi utajisikiaje kunyanyua kombe hilo ambalo limekuwa likililiwa kwa muda mrefu na mashabiki wa timu yako?

Itakuwa ni historia nzuri sana kwa upande wangu kama itakuwa hivyo, kwasababu Mungu ndiyo anajua nini kipo mbele yetu. Kwa upande wangu aitakuwa ni historia ya aina yake kwasababu tumekaa kipindi kirefu bila kuchukua ubingwa.

Kufutwa kwa kadi nyekundu Yanga vs Simba

Kwenye mechi iliyopita ya watani wa jadi ulipewa kadi nyekundu lakini baadae ikafutwa, ulipokeaje uamuzi wa kufutwa kwa ile kadi?

Ilikuwa ni faraja kwangu kwasababu haki ilitendeka, kabla ya hapo wengi walidhani kuna kitu nilimfanyia mwamuzi lakini sikufanya chochote, walipoangalia vizuri wakagundua refa ndiyo mwenye makosa. Na hiyo ni kuwadhihirishia wote waliodhani nilimfanyia refa kitu kibaya. Mimi kama nahodha siwezi kufanya hivyo kwasababu naongoza wachezaji wenzangu uwanjani.

Nilimfata mwamuzi ili kumuuliza kuhusiana na goli tulilofungwa lakini sikufanya chochote, lakini wakati anarudi nyuma akajikwaa kwenye waya akaanguka akadhani nilimsukuma.

Mkude kutomaliza dakika 90 (Simba vs Yanga) ni mkosi?

Kwa mechi kadhaa za Simba na Yanga umekuwa humalizi dakika 90, kuna mechi uliumia bega ukashindwa kuendelea na mchezo, mechi iliyopita ulitolewa kwa kadi nyekundu ambayo ilifutwa baadae. Unadhani unabahati mabaya na mechi za Simba na Yanga?

Ni moja ya sehemu ya mchezo, chochote kinaweza kutokea huwezi jua Mungu ananiepusha na kitu gani labda ningeendelea ningevunjika au kuna chochote kibaya kingenitokea, kwahiyo huwa silaani.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>