Unaweza kusema kila mtu anatamba nyumbani kwake, hiyo imekuja baada ya shabiki mmoja wa Simba kujikuta akichezea kichapo cha haja baada ya kukatiza kwenye jukwaa la mashabiki wa Tanzania Prisons huku akiwa amevalia uzi mwekundu.
Shabiki huyo alianza kuchezeshewa kisago na kuvuliwa jezi yake ambayo ilitupwa huku yeye akiondoka akiwa na vest.
Jukwaa la mashabiki wa Tanzania Prisons lilipewa support ya nguvu na mashabiki wa Yanga pamoja na baadhi ya mashabiki wa Mbeya City ambao waliamua kuonesha uzalendo kwa kuishangilia timu hiyo ya jeshi la magereza mkoni Mbeya.
Mara kadhaa imetokea kwenye uwanja wa taifa shabiki wa Simba au Yanga kupigwa au kuchaniwa jezi yake pinfi anapokatika kwenye jukwaa waliopokaa mashabiki wa timu pinzani, kwenye mechi ya Prisons na Simba yakamkuta shabiki wa mnyama.
Lakini shabiki huyo alifanikiwa kukimbia kabla hajaumizwa licha ya polisi kushindwa kumsaidia kwasababu ya kutenganishwa na uzio unaotenganisha mashabiki kutoka kwenye eneo la pitch.