Kamera ya shaffihdauda.co.tz ilifanikiwa kuzinasa picha mbili za makocha Joseph Omog na Meja Mingange kabla na baada (before and after) ya mchezo wa Tanzania Prisons na Simba uliochezwa kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Kocha wa Simba Joseph Omog anaonekana mwenye furaha na amani kabla ya kuanza kwa mchezo wakati anasalimiana na kocha wa Tanzania Prisons Meja mstaafu Abdul Mingange.


Baada ya mchezo Omog anaonekana aliyepoteza furaha yake ya awali baada ya kupoteza game ya pili mfululizo kwa kufungwa na Tanzania Prisons.
