Kila mwanadamu ana siku ambayo ni muhimu kwake, lakini sote tunaungana kwa pamoja katika siku moja ambayo ni muhimu kwetu kwa pamoja nayo ni niku ya kuzaliwa.
Siku hii ni muhimu kwa kila mwanadamu kwasababu ndiyo siku pekee iliyomfanya aishi kwenye ulimwengu huu bila kujali ni aina gani ya maisha atakayo kutana nayo, yawe ni ya raha au taabu.
Wachezaji wa klabu ya Simba SC Boniphace Maganga na Hamisi Kiiza, jana walisherehekea kuadhimisha siku zao za kuzaliwa ikiwa ni Octoba 16, 2015. Katika hafla hiyo fupi iliyofanyika baada ya mazoezi ya Simba yaliyofanyika kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, zilipigwa picha kadhaa zikionesha matukio tofauti wakati wa hafla hiyo.
Mtandao huu unawatakia kila la heri wachezaji hao katika maisha yao ya soka na nje ya uwanja pia.
Hizi ni baadhi ya picha za matukio muhimu yaliyotokea wati Kiiza na Maganga wakiadhimisha siku za kuzaliwa kwao.